July 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Usimamizi mbovu wa rasilimali chanzo cha umaskini

Mkazi wa Mji mdogo wa Mirerani, Asha Saidi akichekecha mchanga kwenye machimbo ya madini ya Tanzanite

Spread the love

USIMAMIZI  mbovu wa rasilimali za nchi umetajwa kuwa chanzo cha umasikini, licha ya Tanzania kuwa na utajiri wa rasilimali za madini, gesi na wanyama pori bado rasilimali hizo hazijaweza kubadilisha maisha ya Watanzania na hata huduma muhimu za kijamii kama maji,afya na barabara. Anaandika Ferdinand Shayo, Mererani … (endelea).

Hayo yameelezwa na Mlezi wa Vicoba mji mdogo wa Mirerani, Peter Toima ambaye pia ni kada wa Chama cha Mapinduzi anayegombea nafasi ya Ubunge jimbo la Simanjiro alipozindua shirikisho la vikundi hivyo amesema kuwa mji wa Mirerani unakabiliwa na changamoto nyingi za ukosefu wa huduma ya maji safi na salama ya uhakika, pamoja na miundombinu mibovu licha ya utajiri mkubwa unaopatikana katika ardhi hiyo na kujulikana kwa uchimbaji wa madini ya  Tanzanite dunia nzima.

Toima amesema kuwa fursa ya upatikanaji wa madini hayo inapaswa kubadilisha uchumi wa mji wa Mererani na Tanzania kwa ujumla tofauti na hali ilivyosasa watu wachache wananufaika na fursa hiyo.

Mwanachama wa Vicoba Jafary Matibwa  ameiomba serikali na mashirika binafsi yavisaidie vikundi vya Vicoba  ili kuimarisha uchumi kuanzia ngazi ya  familia,jamii na taifa kwa ujumla.

Hellen Joseph na Ernest Mola wameeleza kuwa  uchimbaji wa madini ya Tanzanite unapokua mzuri wanafanya biashara kwa zao kwa uhakika na kupata faida pia wameeleza kunufaika na kuwa moja kati ya wanachama wa Vicoba  kwani imewasaidia kuendesha familia zao,kusomesha watoto na kufungua biashara.

Kwa muda mrefu vikundi vya hivyo  vimekua ni mkombozi wa Wanawake na Wanaume ambao wamekua wakipiga vita umasikini na kujikomboa kiuchumi na hata kujiajiri.

error: Content is protected !!