July 29, 2021

Uhuru hauna Mipaka

‘Usiku watoto wasitumwe nje’

Spread the love
JAMII imeshauriwa kuacha tabia ya kutuma watoto nje wakati wa usiku ili kuwaepusha na matatizo ya ukatili wa kijinsia ikiwemo kubakwa na kulawitiwa, anaandika Christina Haule.
Khasim Munga, Kaimu Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Mlumbiro, Kata ya Mtibwa wilayani Mvomero mkoani Morogoro amesema hayo kwenye mdahalo wa wazi wa kuwaelimisha wanafunzi juu ya masuala ya kupinga ukatili wa kijinsia kwenye mradi wa kupinga ukatili wa kijinsia (GEWE II).
Mradi huo umeandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA) kwa ufadhili wa Shirika la Msaada la Denmark (DANIDA) na kufanyika wilayani humo.
Munga amesema kuwa, watoto wanapaswa kupewa uangalizi hasa waakati wa usiku kufuatia kuwepo kwa uwezekano mkubwa wa kukumbwa na masuala ya ukatili wa kijinsia.
Asha Halfani akizungumzia juu ya suala la ukatili wa kijinsia mjumbe wa kamati ya taarifa na maarifa iliyoandaliwa na TAMWA katika Kijiji cha Kunke wilayani humo amesema,  wakiwa wapambanaji wa masuala hayo huwasaidia wanawake na jamii zinazokumbwa na ukatili na kufikia hatua ya kuona manufaa ya mradi huo.
Ameiomba serikali kuweka nguvu zaidi katika suala la uangalizi wa wazazi wa kike wanaotelekezwa wakiwa na watoto wadogo wanaohitaji msaada.
error: Content is protected !!