Friday , 29 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Ushirikiano wa EWURA, Wizara ya Madini waokoa Bil 121.6
Habari Mchanganyiko

Ushirikiano wa EWURA, Wizara ya Madini waokoa Bil 121.6

Noti za Elfu Kumi
Spread the love

EWURA kwa kushirikiana na Wizara ya Nishati na Madini iliandaa Mfumo wa Uagizaji wa Pamoja (BPS) wa mafuta nchini, Utafiti wa UDSM, Aprili 2014, ulibaini kuwa Jumla ya fedha zilizookolewa ni sh.bilioni 121.6 kwa  mwaka 2012 na 2013. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Hayo yamebainishwa na Kaimu Mkurugenzi wa EWURA, Nzinyagwa Mchany wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa sambamba na kueleza kuwa kwa sasa mamlaka hiyo imehamishia makao yake Jijini Dodoma.

Aidha ili bainisha kuwa kupungua kwa gharama za usafirishaji na Premium ni Sh. 81.9 bilioni katika kipindi cha miaka miwili, kupungua kwa gharama za demurrage  kwa Sh. 25.7 bilioni na Kupungua kwa “ocean losses” kwa Sh. 14 bilioni baada ya kubadilisha taratibu za uagizaji mafuta kutoka “Cost, Insurance and Freight” na kuwa “Delivery at Port.”

Katika hatua nyingine alisema kuwa EWURA inakabiliwa na changamoto ya kuchelewa utoaji wa leseni za ujenzi wa vituo vya mafuta.

Aidha alisema kuwa changamoto nyingine ni wawekezaji kutokamilisha masharti ya leseni hususan kibali cha matumizi ya ardhi na kibali cha mazingira.

“Hata hivyo alisema kuwa  EWURA inaendelea kutoa elimu kuhusu ukamilifu wa vigezo vya kupata leseni,” alieleza Mchany.

Akizungumzia tathimini ya uthibiti Mchany, amesema kuwa Mwaka 2011, utafiti uliodhaminiwa na Umoja wa nchi za Ulaya, ulibainisha kuwa EWURA ni miongoni mwa wadhibiti wa mfano katika Afrika kwa vigezo vya utawala bora na maudhui ya kiudhibiti.

Alisema kwamba mwaka 2009 na 2010, EWURA ilifanya vizuri kwenye Mapitio Rika (Peer Reviews) yaliyoendeshwa na Chuo Kikuu cha Cape Town kwa wadhibiti wa umeme kati ya nchi za Uganda, Kenya, Zambia, Namibia na Ghana.

Wakati huo huo, EWURA imesema kuwa imeweka mkakati kabambe wa kukabiliana  na kuwachukulia hatua kali wale wauzaji wa gesi ya majumbani ambao hawana mizani ya kupimia uzito wa mitungi ya gesi.

Kwa mujibu wa mkuu wa kitengo cha habari na Mahusiano, EWURA, Titus Kaguo, watakaobainika kukiuka sheria zilizowekwa na mamlaka hiyo watatozwa faini ya kuanzia Sh. 3 hadi 5 milioni.

“Kila amtu ambaye anauza au kusambaza gesi ya matumizi ya majumbani anatakiwa kuwa na mzani kwa ajili ya kupimia uzito wa mitungi ya gesi na kutokuwa na mzani ni kosa na iwapo mtu huyo atakamatwa atalazimishwa kutozwa faini,” amesema.

Aidha, amesema kuwa watanzania na jamii kwa ujumla wake wanatakiwa kujiepusha na ubebaji wa mafuta ya Petroli katika vifaa vyenye hasili ya plasitiki kwani kwa kutumia vifaa hivyo ni hatari kwa usalama wao na siyo vyombo sahihi kubebea bidhaa hiyo.

Akizungumzia suala la uwepo wa uchakachuaji wa mafuta ya Petroli, Kaguo amesema kuwa suala hilo kwa sasa limepungua kwa kasi kubwa kutoka asilimia 78 mwaka 2007 hadi kufikia asilimia 4 mpaka mwaka huu katika nchi nzima.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mtandao watetezi wa haki za mazingira Tanzania waundwa

Spread the loveMTANDAO wa watetezi wa haki za mazingira nchini Tanzania, umeundwa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga kuongoza usambazaji wa mitungi ya gesi 10,000 ya Taifa Gas

Spread the loveNaibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga ameahidi kuongoza kwa ufanisi...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyabiashara, wawekezaji China waridhia kuwekeza bil. 800 katika sekta 5 nchini

Spread the loveUJUMBE wa wafanyabiashara na wawekezaji wakubwa kutoka Jimbo la Changzhou...

Habari Mchanganyiko

Bil. 4.42 kumaliza uhaba maji kata 2 Musoma Vijijini

Spread the loveWANANCHI wa kata za Busambara na Kiriba, Jimbo la Musoma...

error: Content is protected !!