Thursday , 2 February 2023
Home Kitengo Michezo Ushindi waiibua Simba, yawatupia kijembe watani zao
Michezo

Ushindi waiibua Simba, yawatupia kijembe watani zao

Spread the love

 

UONGOZI wa timu ya Simba ya jijini Dar es Salaam nchini Tanzania imewashukuru mashabiki kwa kuchagiza ushindi wa 3-1 wa dhidi ya Asec Mimosas ya Ivory Coast kwenye mchezo wa makundi wa Kombe la Shirikisho Afrika. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Simba iliibuka na ushindi huo mkubwa jana Jumapili, katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam. Magoli hayo yalifungwa na Pape Sakho, Shomari Kapombe kwa penati pamoja na Peter Banda.

Taarifa ya Simba iliyotolewa leo Jumatatu, tarehe 14 Februari 2022 imewaomba mashabiki zao kutowasumbua mashabiki wengine wanaofika uwanjani kushuhudia michezo yao.

“Ukweli ni kwamba mashabiki wa timu nyingine wanakuja kwenye mechi zetu kufuata burudani ambayo hawaipati kwenye timu zao hivyo ni vema kuwapokea na kuwapa mazingira mazuri ya kufurahia kabumbu safi kutoka Simba,” imeeleza taaifa hiyo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

GGML: Uwanja mpya wa Geita Gold FC kukamilika Mei, 2023

Spread the loveUWANJA wa Magogo unaojengwa na Halmashauri ya Mji wa Geita...

Michezo

Wanafunzi chuo Mwalimu Nyerere wapongezwa kwa ushindi

Spread the love  UONGOZI wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA)...

Michezo

Arsenal waipopoa Manchester United

Spread the loveKLABU ya Arsenal inayoshiriki Ligi Kuu England imewatandika Mashetani Wekundu...

Michezo

Mchezaji Singida apoteza maisha mazoezini

Spread the love  MCHEZAJI na kapteni wa timu ya vijana ya Singida...

error: Content is protected !!