Sunday , 2 April 2023
Home Kitengo Habari Kimataifa Ushindi wa Biden: Korea, China ‘zakuna  vichwa’
Kimataifa

Ushindi wa Biden: Korea, China ‘zakuna  vichwa’

Joe Biden, Rais Mteule wa Marekani
Spread the love

WAKATI dunia ikidhani imepumua baada ya Donald Trump, Rais wa Marekani (2016-2020) kuangushwa, China na Korea Kaskazini zinaweza ‘kukasirishwa’ na uamuzi wa raia wa Marekani. Inaripoti Shirika la Utangazaji la BBC … (endelea).  

Joe Biden, Rais Mteule wa Marekani anayetarajiwa kuanza kazi kwenye Ikulu ya nchi hiyo tarehe 20 Januari 2021, anayo historia inayoumiza Taifa la China na Korea Kaskazini.

Korea Kaskazini

Kim Jong Un, ni miongoni mwa viongozi wa dunia asiye na haja na Biden, wawili hawa waliingia kwenye  msuguano mkali wakati  Biden akitumika kama mtaalamu wa masuala ya Mambo ya  Nje wa Marekani.

Mzozo mkali kati ya Kim na Marekani, ulimsukuma Kim kumwita Biden ‘mbwa koko,’ hiyo ni moja ya kauli kali aliyoitoa Kim kwa viongozi wa Marekani.

Kim pamoja na mbwembwe pia maneno mengi ya Trump, kwake ni bora kuliko kukutana na Biden anayeonekana kuwa na akili nyingi katika masuala ya uhusiano wa kimataifa.

Kim hakumjali sana Trump kwa kuwa, alimuona ni muongeaji zaidi na mropokaji ‘asiyejua’ athari za kile anachokisema kama kiongozi  mkubwa duniani, lakini kwa Biden, akili ya Kim inajichekecha upya kutokana na historia yake.

Ni wazi kwamba Kim angependelea tena muhula mwengine wa miaka minne ya Trump.

Mikutano ya viongozi hao wawili ilileta picha za kihistoria, lakini hakuna kitu kikuu kilichoafikiwa. Hakuna hata pande moja iliopata kile ilichokuwa ikitarajia.

Korea Kaskazini imeendelea kujenga silaha za kinyuklia na Marekani imeendelea kuiwekea vikwazo.

Badala yake, Biden ametaka Korea Kaskazini kuonesha kwamba, ipo tayari kuacha utengenezaji wa silaha za kinyuklia kabla ya kufanya mikutano yoyote na Kim.

Wachambuzi wanasema, kwamba iwapo Biden hatoanzisha mazungumzo ya haraka na kiongozi huyo, huenda hali ya chuki kati ya mataifa hayo mawili ikarejea.

China

Unaweza kufikiria kwamba Beijing ingelifurahia sana iwapo Trump angeshindwa.

Alikuwa kiongozi wa mstari wa mbele kuikashifu China mara kwa mara na kuiwekea vikwazo kadhaa mbali na kuilaumu kwa virusi vya corona.

Lakini wachambuzi wanasema, uongozi wa China huenda sasa unahisi kutofurahishwa na kushindwa kwake. Sio kwasababu wanampenda bali kwasababu alikuwa anaiharibu Marekani na kuvunja uhusiano wa taifa hilo na mataifa mengine.

China ilidhani kwamba, muhula mwengine wa Trump ungeliporomosha uchumi wa Marekani na kusababisha kuanguka kwa uwezo wake.

Kuchonganishwa kwa Marekani na mataifa mengine hata yale aliyonayo jirani, mfano Mexico kunaifanya China kujisogeza na kujenga urafiki nayo.

Lakini uwepo wa Biden unaifanya China kutofurahia zaidi kwa kuwa, ndio mwanasiasa aliyebobea katika masuala ya kujenga urafiki na malengo kwa taifa hilo.

China inaamini, uhusiano mbaya wa Marekani na mataifa mengine ulilifanya Taifa (China) hilo kuongeza mwendo katika kujijenga kiuchumi. Kwa China, ushindi wa Biden ni pigo katika harakati zake za kujijenga nje ya mipaka yake.

Biden ameshinda kwa kura za majimbo 290 wakati Trump akipata kura 214. Ni kura 270 za majimbo zilizohitajika kumfanya mgombea mmoja kuibuka na ushindi.

Licha ya Biden kumvuruga Trump kwenye kura za majimbo, pia kamtwanga kwenye kura za wananchi (popular votes).

Biden amepata kura 74,566,731 sawa na asilimia 50.5 huku Trump akipata kura 70,396,573 sawa na asilimia 47.7 ya kura zilizopigwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Kimataifa

Marekani yatia mguu maaandamano Kenya, yatoa maagizo kwa Rais Ruto, Odinga

Spread the love  Mabalozi kutoka nchi sita za Magharibi, zikiongozwa na Marekani,...

Kimataifa

Papa Francis alazwa hospitali kutokana na maambukizi ya mapafu

Spread the love  KIONGOZI wa Kanisa katoliki duniani, Papa Francis jana Jumatano...

Kimataifa

Nyumba ya babu yake Makamu wa Rais wa Marekani yatafutwa Zambia

Spread the love  KAMALA Harris, makamu wa rais wa Marekani, amepanga kutembelea...

Kimataifa

Benki ya Uswizi mbioni kuziwekea vikwazo akaunti za siri za Wachina

Spread the love  WAKATI Serikali na Benki ya Uswizi ikichukua hatua kali...

error: Content is protected !!