Sunday , 29 January 2023
Home Kitengo Michezo Ushindi mabao 5 Ureno, Ronaldo aweka rekodi mpya
Michezo

Ushindi mabao 5 Ureno, Ronaldo aweka rekodi mpya

Spread the love

 

NAHODHA wa Timu ya Taifa ya Ureno na Staa wa Manchester United Cristiano Ronaldo, ameweka rekodi mpya mara baada ya kupachika mabao matatu (Hat Trick), kwenye ushindi wa mabao 5-0, walioupata timu yake ya Taifa dhidi ya Luxembourg. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Mchezo huo wa kundi A, wa kusaka tiketi ya kufuzu kwa Fainali za kombe la Dunia, zitakazofanyika Qatar 2022, huku mabao mengine ya Ureno yakiwekwa kimyani na Bruno Fernandes na Joao Palhinha.

Rekodi iliyowekwa na mchezaji huyo, ni kufikisha Hat Trick 58, katika maisha yake yote, toka alipaonza kucheza soka la kulipwa.

 Aidha ya rekodi ya mchezaji huyo haukuishia hapo tu, bali aliandikisha Hat trick yake ya 10 akiwa na timu ya taifa ya Ureno, katika michezo 180 aliyocheza na kuweka rekodi nyingine ya kuwa mfungaji bora wa muda wote, mara baada ya kupachika mabao 111.

Katika kusaka tiketi za kufuzu fainali hizo, Ronaldo akiongoza timu ya Taifa ya Ureno, mpaka sasa wamefikisha jumla ya pointi 16, katika michezo sita waliocheza.

Ronaldo pia amekuwa kinara wa upachikaji mabao, katika michezo ya kusaka tiketi ya kushiriki kombe la Dunia, kwa kupachika mabao 36, katika michezo yote aliyocheza.

 

 

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

GGML: Uwanja mpya wa Geita Gold FC kukamilika Mei, 2023

Spread the loveUWANJA wa Magogo unaojengwa na Halmashauri ya Mji wa Geita...

Michezo

Wanafunzi chuo Mwalimu Nyerere wapongezwa kwa ushindi

Spread the love  UONGOZI wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA)...

Michezo

Arsenal waipopoa Manchester United

Spread the loveKLABU ya Arsenal inayoshiriki Ligi Kuu England imewatandika Mashetani Wekundu...

Michezo

Mchezaji Singida apoteza maisha mazoezini

Spread the love  MCHEZAJI na kapteni wa timu ya vijana ya Singida...

error: Content is protected !!