January 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Usalama wa Taifa wawadhalilisha wapambe wa wabunge

Spread the love

WAPAMBE wa Wabunge na Wabunge ambao walikuwa wakiapishwa mjini Dodoma katika Bunge la 11 wameulalamikia utaratibu mbovu uliowekwa na Bunge kwa kuwazuia baadhi ya wapambe wao kutoingia ndani ya ukumbi wa bunge kwa ajili ya kuwashuhudia wabunge wao wakiapishwa. Anaandika Dany Tibason, Dodoma … (endelea).

Mbali na hilo walilalamikia hatua ya Usalama wa Taifa ambao walikuwa wakiwapokea wageni hao kwa kutumia lugha chafu huku wengine wakiwatuhumu usalama hao kwa kuwapiga baadhi ya wapambe makofi.

Mmoja wa wabunge ambae alikerwa na tukio hilo ni mbunge wa viti maalum ni Conchester Rwamlaza (Chadema) ambaye amesema wapambe wake kutoka Mkoani Kagera kushindwa kuingia ndani kushuhudia jinsi anavyoapishwa.

Amesema utaratibu ambao umewekwa na bunge msimu huu ni tofauti na miaka mingine kwani mwaka huu urasimu umekuwa mkubwa.

Kwa upande wa wapambe wakiwa nje ya viwanja vya bunge walisikika waliwalalamikia maofisa usalama wa mlango wa kuingilia wageni kwa kauli zao mbaya za kuwadharirisha wageni wa wabunge ambao walikuja kwa ajili ya kuwashuhudia wabunge wao wakiapishwa.

Matukio hayo ambayo yaliwakera wapambe na wabunge yalitokea siku ya kwanza ya kuwaapisha wabunge huku ikitajwa kuwa katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashilillah kuingilia kati kuzuia hali hiyo na kubadilisha utaratibu.

Inaelezwa kuwa katibu wa Bunge alitoka ndani ya ukumbi wa bunge na kubadilisha utaratibu kwa kuwataka wapambe wa wabunge waruhusiwe kuingia ndani ya bunge na mara mbunge anapomaliza kuapishwa anatoka ukumbini na wapambe wake ili kuwapisha wengine waingie.

Jambo lingine ambao lilionekana kuwa la tofauti katika maeneo ya nje ya ukumbi wa bunge ni wapambe wa wabunge wa vyama vya upinzani wanaounda umoja wa Katiba ya Wananchi, (Ukawa) walionekana kushangilia huku wale wa chama tawala wakionekana kupigwa bumbuwazi.

Katika maeneo ya ukumbi wa bunge katika mlango wa kuingilia wageni wabunge wa upinzani walionekana kuwa na shamrashamra zaidi kwa kuimba nyimbo za kuikebei CCM na kuwapongeza wabunge wao huku wabunge wa CCM akiwemo mbunge wa Ilamba Mwiguru Nchemba (CCM) na mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu (CCM) wakionekana kuwa wamepooza katika maeneo hayo.

Kivutio zaidi ni wapambe wa kutoka Longido na Mbozi ambao walionekana kuimba nyimbo mbalimbali za kijigamba kwa kuwaondoa wakongwe bungeni ikiwa ni pamoja na wabunge kutoka Bunda.

Katika hatua nyingine mji wa Dodoma umeonekana kuwa na msongamano mkubwa wa magari na watu tofauti na mikoa kipindi kingine chochote huku bei ya bidhaa mbalimbali zikiwa zimepanda hususani vyumba.

Wabunge wanena

Kwa hatua nyingine mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu (Chadema) na mwanasheria wa chama hicho amejigamba kuwa hakuna bunge zuri na la maana zaidi kwa watanzania kama Bunge la 11.

Amesema bunge hilo ni zuri kutokana na kuwa kuwepo kwa vijana wengi vijana ambao wanajitambua na wenye uchungu na maisha ya wananchi.

Lissu amesema pamoja na ujanja ya CCM ya kutaka kuweka viongozi wanaowakata katika nafasi mbalimbali kama vile uspika, unaibu spika na mwanasheria mkuu kwa lengo la kulinda maslahi yao lakini ni wazi kuwa wapinzani watakabiliana nao kisawasawa.

“Bunge hili ni bunge zuri kweli kweli kwanza lina wabunge wengi vijana na upinzani wapo wengi sana wa kutosha hivyo tutakabiliana nao kwa hoja na sasa hatoki mtu ndani ya ukumbi wa bunge.

“Unajua hawa watu ni wa ajabu sana ukitoka tu wanatumia mwanya huo kufanya mambo yao ambayo yanaliingiza taifa katika hasara kubwa zaidi sasa kazi tutaifanya na wananchi watafurahi,” amesema Lissu.

error: Content is protected !!