January 17, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Usajili Yanga usipime, GSM kumwaga tena pesa

Mhandisi Hersi Said, Mkurugezni wa uwekezaji Gsm

Spread the love

 

KUELEKEA kumaliza kwa msimu wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2020/21, wafadhiri wa Yanga, Kampuni ya GSM, wameahidi kumwaga fedha kwa ajili ya usajili wa msimu ujao kwa kushusha wachezaji wa maana ndani ya msimu ujao. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Hayo yalitanabaishwa wazi na Mkurugezni wa uwekezaji wa kampuni hiyo, Mhandisi Hersi Said, kwenye Mkutano Mkuu wa mwaka wa klabu hiyo, uliofanyika jana kwenye ukumbi wa DYCC-Temeke, Dar es Salaam.

Hersi ambaye pia ni Mwenyekiti wa kamati ya mashindano ya klabu hiyo, ambaye aliongea kwa niaba ya Mkurugenzi wa Kampuni ya GSM, Gharib Said Mohammed, na kutoa salamu zake kwa kusema kuwa tajiri huyo atafanya kila liwezekanalo kuinua timu hiyo na kuwa tishio ndani ya bara la Afrika.

“Napenda kuwapa neno la faraja wana Yanga, najua mabadiliko haya yatachukua muda, GSM amesema atafanya kila liwezekanalo kuiinua timu ili kuwa moja ya timu bora katika Afrika.

“Yale tuliyoyafanya msimu huu, na msimu unaofuata tumeaanza kufanya jitihada kubwa kuifanya Yanga kuwa bora kuliko timu yoyote na sio Tanzania tu, bali Afrika,” alisema.

Aidha Hersi aliongezea kuwa bosi huyo ameweka pesa kwa ajili ya usajili, pamoja na kambi ili kuifanya timu hiyo kuwa ya kipekee na yakuigwa ndani ya bara la Afrika.

“Kwa nafasi yake ameiweka pesa kwa ajili ya kufanya usajili bora, pamoja na kambi na kuhakikisha klabu hii inakuwa sehemu ya kuigwa barani Afrika,” aliongezea.

Wakati mipango hiyo ikiendelea tayari klabu hiyo imeshaanza usajili na kufanikiwa kumnyaka mlinzi wa kulia wa klabu ya AS Vita ya Congo, Djuma Shabani.

Licha ya usajili huo, lakini pia Yanga wapo kwenye hatua ya mwisho kukamilisha usajili wa kiungo mshambuliaji wa klabu ya Dodoma Jiji, Dickson Ambundo.

error: Content is protected !!