BAADA ya Mwanariadha Usain Bolt wa Jamaika kutamba katika mbio fupi duniani na kuweka rekodi kadhaa ameamua kugeukia mchezo wa soka baada ya kusaini kandarasi ya kuichezea klabu ya Mamelods Sundowns ya nchi Afrika ya Kusini. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).
Bolt ambaye ndiye binadamu mwenye kasi zaidi duniani alikuwa na ndoto ya kucheza soka muda mrefu huku akitajwa mara kadhaa kutaka kuichezea klabu ya Manchester United.
Wadau wengi wa soka wanasubiri kuona uwezo aliouonyesha katika medani ya riadha katika mbio za mita 100 na 200 atauhamishia katika soka ndani ya Ligi Kuu ya Afrika Kusini na michuano ya kimataifa ambayo timu yake mpya itashiriki.
Bolt amekabidhiwa jezi namba moja iliyozoeleka kutumiwa na makipa, lakini akiwa katika klabu hiyo ataitumia akiwa mchezaji wa ndani.
Leave a comment