Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Usafiri wakwamisha kesi ya Rugemalira, Seth
Habari za SiasaTangulizi

Usafiri wakwamisha kesi ya Rugemalira, Seth

Spread the love
TATIZO la usafiri limekwamisha kesi ya Harbinder Seth na mfanyabiashara James  Rugemalira iliyokuwa ikitajwa leo Alhamisi Novemba 22, 2018 lakini imeshindikana kutoka na washitakiwa hao kutokuwepo mahakamani. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi amesema kesi hiyo imeshindwa kutajwa kutokana na Rugemalira na Seth kushindwa kuwepo mahakamani kutokana na shida ya usafiri. Washtakiwa hao wanaokabiliwa na mashtaka 12 ya uhujumu uchumi ikiwamo ya utakatishaji wa fedha.

Wakili wa Serikali Emmanuel Nitume amesema mahakamani kuwa washtakiwa wote wanaokabiliwa na kesi hiyo hawapo kwa sababu kuna shida ya kusafiri, lakini pia ofisa mmoja wa Jeshi la Magereza aliyekuwepo mahakamani hapo alisisitiza jambo hilo la shida ya usafiri.

Katika maelezo yake Nitume amedai kesi hiyo ilipangwa kwa ajili ya kutajwa, upelelezi wake bado unaendelea na akaomba ipangiwe tarehe nyingine ya kutajwa. Baada ya kusikiliza maelezo hayo Hakimu Shaidi ameahirisha kesi hiyo hadi  Desemba 6, 2018.

Washtakiwa hao  wanakabiliwa na mashtaka  12 ya  uhujumu uchumi  kwa kula njama, kujihusisha na mtandao wa uhalifu, kughushi,  kutoa nyaraka za kughushi, kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu,  kutakatisha fedha  na kuisababisha hasara ya Dola 22milioni za Marekani na Sh 309,461,300,158.27.

 

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Habari za SiasaTangulizi

Tanzania, Uturuki zanuia kukuza biashara, uwekezaji

Spread the loveSERIKALI za Tanzania na Uturuki zimekubaliana kuendeleza dhamira ya kuimarisha...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza ajira watendaji daftari wapiga kura

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza nafasi...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema yatangaza ruti awamu ya pili maandamano

Spread the love  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema awamu ya...

error: Content is protected !!