Spread the love

 

UONGOZI wa la Dodoma nchini Tanzania, umesema hautasita kumchukulia hatua za kisheria mtu ambaye anakwamisha juhudi za maendeleo sambamba na utunzaji wa mazingira na usafi. Anaandika Danson Kaijage…(endelea).

Angalizo hilo limetolewa na mkurugenzi mtendaji wa Jiji la Dodoma, Joseph Mafuru alipokuwa akizungumza na wakazi wa Kata ya Makole wakati wa kufanya usafi na kuondoa vibanda visivyo kuwa rasmi katika eneo hilo.

Mafuru amesema Dodoma ni makao makuu ya nchi hivyo kunatakiwa kuwepo na usafi wa hali ya juu na kwa misingi hiyo kwa sasa sheria ndogo zitafuatwa bila kumwonea mtu au kufanya ubaguzi.

Akiwa na wakazi hao eneo la makole maarufu kama CBE, Mafuru amesema maeneo yote ambayo ni hifadhi ya barabara yatafanywa kuwa sehemu ya upandaji wa miti ya kivuli, matunda pamoja na maua.

Aidha, katika harakati za kuhamikisha Jiji la Dodoma linakuwa safi wataweka maeneo muhimu na yenye miundombinu rafiki ya wafanyabiashara ndogondogo badala ya kukaa katika maeneo ambayo siyo rasm.

Katika hatua hiyo, Mafuru amesema tayari wameisha tangaza tenda ya kumpata mzabuni wa kuzoa taka na kampuni nne zimepatikana.

Amesema kampuni ya kwanza ya Green Waste imelazimika kuvunja mkataba na jiji kutokana na kushindwa kutimiza majukumu yake ukusanyaji wa taka.

“Kutokana na hali hiyo Jiji ilichukua hatua za haraka Kwa kukodisha magari nane ya kusaidia kuzoa taka katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dodoma.

“Pamoja na kukodisha magari ya kuzoa taka kwa saa tayari imeisha tangazwa zabuni na malampuni ya kuzoa taka yataanza hivi karibuni”amesema Mafuru.

Naye mkuu wa idara ya mazingira na uthibiti wa taka ngumu, Dickson Kimaro amewaomba Watanzania hususani wana Dodoma kutunza mazingira kwa kupanda miti na na maua katika maeneo yao.

Kimaro amesema ni wajibu wa kila mtanzania husususani wanadodoma kwa kuhakikisha anatunza mazingira kuanzia nyumbani.

“Nataka kuwambia waanchi wa Dodoma lazima tujenge utamaduni wa kutunza mazingira na usafi uanzie nyumbani kwako.

“Tunatamiwa kujenga utamaduni wa kufanya usafi mara kwa mara bila kusubiri muambiwa na ili uwe msafi ni lazima pia hata malezi ya watoto yawe ya muwajengea misingi mizuri ya utunzaji wa mazingira na u safi,” amesema Kimaro.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *