Friday , 29 March 2024
Kimataifa

Urusi yaivamia Ukraine

Spread the love

 

NCHI ya Urusi, imeanzisha rasmi mapigano ya kijeshi katika mikoa ya mashariki ya Ukraine, baada ya Rais wake, Vladimir Putin kutangaza operesheni ya kijeshi. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

Rais Putin alitangaza operesheni ya kijeshi, mapema leo Alhamisi, akihutubia wananchi kupitia televisheni ya taifa hilo, huku akidai hatua hiyo inalenga kuimarisha amani, katika mikoa iliyotangaza kujitenga na Ukraine.

Katika hotuba yake, Rais Putin aliwaonya wanajeshi wa Ukraine walioko katika eneo la mashariki, yalipoibuka mapigano hayo, kuweka silaha chini.

Taarifa za mitandao ya kimataifa zinadai kuwa, tayari Urusi imetuma vikosi vya kijeshi Ukraine, ambapo vimeanza kurusha makombora kwenye miji kadhaa ya Taifa hilo.

Imeripotiwa kuwa, Jeshi la Anga Ukraine limefanikiwa kuzuia shambulio la anga lililofanywa na Urusi. Urusi ilirusha makombora kwenye Uwanja wa Ndege wa Boryspil, karibu na Mji Mkuu w Ukraine, Kyiv.

Wakati hayo yanajiri, Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky, amemtupia lawama Rais Putin kwa kushindwa kukubali wito wake wa mazungumzo, ambapo alimtafuta kwa njia ya simu bila mafanikio.

Hata hivyo, Rais Zelensky alionya ikiwa Urusi itaishambulia Ukraine, kwa lengo la kuchukua ardhi ya taifa lake na uhuru wa wananchi wake, hawatasita kujilinda.

Rais huyo wa Ukraine amesema, Urusi imerusha makombora ambayo yameharibu miundombinu ya nchi yake.

Mataifa mbalimbali yamelaani vikali hatua ya Urusi kuanzisha mashambulizi ya kijeshi Ukraine, huku Rais wa Marekani, Joe Biden akiahidi kuwashawishi viongozi wa nchi saba tajiri duniani (G7), waiwekee vikwazo nchi hiyo, kufuatia hatua yake ya kuingilia Ukraine.

Mzozo baina ya Urusi na Ukraine ulishika kasi, kufuatia msimamo wa Rais Putin, kutambua uhuru wa mikoa miwili iliyoko mashariki mwa Ukraine, Donestsk na Luhansk, inayodhibitiwa na waasisi wanaotaka kujitenga.

Kwa mujibu wa mtandao wa BBC Swahili, wananchi wa Ukraine wameanza kukimbia makazi yao, baada ya tangazo la Rais Putin, kuanzisha operesheni ya kijeshi nchini mwa.

Ambapo wamekimbilkia kwenye vituo vya treni vya chini ya ardhi, vilivyomo katika Mji Mkuu wa Kyiv.

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoKimataifa

Zuma akataliwa kugombea urais

Spread the loveTUME Huru ya Uchaguzi Afrika Kusini (IEC) imemwondoa rais wa...

KimataifaTangulizi

Zuma akataliwa kugombea urais

Spread the love  TUME Huru ya Uchaguzi Afrika Kusini (IEC) imemwondoa rais...

Habari za SiasaKimataifa

Mwanaye rais jela miaka miaka 6 kwa dawa za kulevya

Spread the loveMwanawe rais wa zamani wa Guinea-Bissau amehukumiwa kifungo cha miaka...

Habari za SiasaKimataifa

Faye aahidi kuongoza kwa unyenyekevu, wagombea wenzie wakubali yaishe

Spread the loveMgombea wa upinzani Senegal, Bassirou Diomaye Faye anajiandaa kuwa rais...

error: Content is protected !!