Saturday , 20 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Urusi yaanza tena mashambulizi nchini Ukraine
Habari Mchanganyiko

Urusi yaanza tena mashambulizi nchini Ukraine

Spread the love

Urusi jana tarehe 16 Julai, 2022 imeanzisha tena mashambulizi yake katika eneo la Donbass Mashariki mwa Ukraine baada ya mapumziko ya muda mfupi ili kupanga tena vikosi vyake. Inaripoti Mitandao ya kimataifa… (endelea)

Wakati wa ukaguzi wa vikosi vilivyohusika katika uvamizi nchini Ukraine, Waziri wa ulinzi wa Urusi, Sergei Shoigu, aliagiza mashambulizi ya kasi ya juu.

Shoigu alitoa maagizo ya kupanua shughuli za makundi ya jeshi la nchi hiyo katika pande zote za mashambulizi.

Wizara huyo wa ulinzi amesema lengo ni kuzuia Ukraine kufanya mashambulizi makubwa ya makombora na silaha dhidi ya miundombinu na raia katika eneo la Donbas na maeneo mengine.

Jeshi la Ukraine limeripoti kuwa limetibua jaribio la mashambulizi ya Urusi kuelekea Bakhmut na karibu na Donetsk katika muda wa masaa 24 yaliyopita.

Mkuu wa jeshi la Ukraine pia amesema baada ya vikosi vya Urusi kujipanga tena, Urusi ilianzisha mashambulizi dhidi ya mtambo wa umeme wa Vuhlehirsk na kwamba mapigano yanaendelea.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Gardner Habash wa Clouds Fm afariki dunia

Spread the loveALIYEKUWA mtangazaji wa kipindi cha Jahazi kinachorushwa na kituo cha...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wauguzi, madaktari 1000 kugawiwa mitungi ya Oryx Gas

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gas na Taasisi ya Doris Mollel Foundation...

Habari Mchanganyiko

Tanzania yachaguliwa Makamu wa Rais Tume ya Shirika la Hali ya Hewa Duniani

Spread the love  TANZANIA kupitia Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA)...

Habari Mchanganyiko

NEMC yaonya wanaojenga bila tathmini ya mazingira

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC),...

error: Content is protected !!