October 23, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Urusi: Ndege iliyoanguka Misri ililipuliwa

Spread the love

URUSI imethibitisha kuwa ajali ya ndege ya Metrojet iliyoanguka na kuua watu zaidi ya 200 katika rasi ya Sinai nchini Misri mwezi uliopita ilikuwashambulizi la kigaidi.

Mkuu wa idara ya usalama wa taifa Alexander Bortnikov amemualeza rais Vladimir Putin kuwa ndege hiyo iliangushwa na bomu lenye uzani wa kilo moja. Bomu hilo lilikuwa sawa na ile yenye viungo vya TNT.

Abiria wote 224 waliokuwa ndani ya ndege hiyo waliangamia. Wengi wao walikuwa ni watalii kutoka Urusi waliokuwa wametokea Sham al Sheikh.

Bortnikov alipokamilisha maelezo yake kwa rais Putin, rais huyo pamoja na mawaziri wengine wakuu waliiunuka na kunyamaza kimya kwa muda kabla ya rais Putin kuapa kulipiza kisasi.

Aidha rais huyo wa Urusi aliapa kuwasaka na kuwaadhibu waliotekeleza mauaji hayo. Putin pia aliapa kuendelea mashambulizi ya ndege nchini Syria.

error: Content is protected !!