Tuesday , 26 September 2023
Home Kitengo Habari Kimataifa Urusi imelipua bwawa kuu la umeme nchini Ukraine
Kimataifa

Urusi imelipua bwawa kuu la umeme nchini Ukraine

Spread the love

SERIKALI mjini Kyiv nchini, Ukraine imeushutumu utawala wa Rais Vladimir Putin wa Urusi, kwa kulipua bwawa lake kubwa katika kituo cha kuzalisha umeme kwa njia ya maji kwenye mto Dnipro, katika eneo la Kherson kusini mwa nchi hiyo. Anaripoti Mwandishi Wetu, kwa msaada wa mitandao ya kijamii….(endelea).

 Bwawa hilo liko katika mji wa Nova Kakhovka, unaokaliwa kwa mabavu na Urusi, ambapo meya aliyewekwa na Moscow ameilaumu Ukraine kwa uharibifu huo.

Hata hivyo, meya huyo anasema, “ni sehemu ya juu ya mtambo pekee ndiyo iliyoharibiwa na makombora; na wala siyo bwawa lenyewe.”

Lakini jeshi la Ukraine limevishutumu vikosi vya Urusi kwa kulipua bwawa hilo kubwa, huku kukiwa na hofu kwamba maelfu ya nyumba zilizo chini ya mto huo sasa zitafurika. Hakuna vyanzo huru vya kuthibitisha madai hayo.

Taarifa ya jeshi la Ukraine inasema, “linachunguza kiwango cha uharibifu.”

Bwawa hilo – Kakhovska (HPP), lililojengwa ya zama za umoja wa Soviet – liko katika mji wa Nova Kakhovka, katika mkoa wa Kherson nchini Ukraine.

Jiji na maeneo mengine kwenye ukingo wa kushoto ya mto Dnipro (mashariki) kwa sasa, yanashikiliwa na Urusi.

Mfereji muhimu wa kubeba maji kutoka Dnipro hadi Crimea inayokaliwa na Urusi, unaoanzia Nova Khakovka, una uwezekano wa kuathirika, pamoja na kituo cha nishati ya nyuklia huko Zaporizhzhia, ambacho kiko kwenye ukingo wa Dnipro karibu kilomita 160 juu ya mto.

Katika taarifa yake asubuhi ya leo, Andryi Yermak, mkuu wa ofisi ya Rais Zelensky, alisema kuwa Urusi itawajibikia kuwanyima maji ya kunywa watu wa Crimea na kuongeza kuwa vitendo vya Urusi “vinatishia ZNPP” (kinu cha nyuklia cha Zaporizhzhia).

Huku hayo yakijiri, habari zaidi zinasema Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ameitisha mkutano wa dharura wa baraza la usalama na ulinzi la taifa la nchini mwake.

Oleksiy Danilov, ambaye ni katibu wa baraza hilo, alisema kwenye Twitter, kwamba mkutano huo ulikuwa unafanyika “kuhusiana na mlipuko wa bwawa la Kakhovsky.”

Taarifa za hivi punde zinasema, maji yanafurika kwenye mto Dnipro na inasemekana yanatishia kusababishia mafuriko makubwa mjini Kherson.

Shughuli ya uokoaji inafanyika katika eneo hilo huku watu wasiopungua 16,000 wakiwa hatarini kutokana na mafuriko hayo, gavana wa Ukraine amesema.

Kinu cha nyuklia cha Zaporizhzhia kinategemea maji ya mto huo kupoza vinu vyake. Hali ya huko kwa sasa inasemekana kudhibitiwa. Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki (IAEA), linasema linafuatilia kwa karibu sakata hilo.

Wakazi katika maeneo yaliyo lwenye hatari wanahamishwa kwa mabasi hadi Kherson, kisha watahamishwa hadi miji tofauti nchini kote ikiwa ni pamoja na mji mkuu, Kyiv, Prokudin anasema katika chapisho la telegram.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Kimataifa

Uvamizi wa kijeshi Milango ya bahari ya Taiwan G7 yapinga China

Spread the loveMKUTANO wa Mawaziri wa Mambo ya nje wa nchi za...

Kimataifa

Rais Kagame kuwania muhula wa nne

Spread the loveRais wa Rwanda, Paul Kagame amesema atawania muhula wa nne...

Kimataifa

Ukraine kufungua kituo cha nafaka Kenya

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto amesema serikali ya Ukraine inapanga...

Kimataifa

Kufungwa kwa mpaka wa Tibet kulivyoathiri maisha ya Wanepali katika vijiji vya milimani

Spread the love  KALU Dhami kutoka Dhalain moja ya kata ya Manispaa...

error: Content is protected !!