August 18, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Urefu wa Fellain haukumsaidia Mourinho

Marouane Fellaini

Spread the love

BAADA ya kutoka sare katika mchezo wa jana wa Ligi Kuu England dhidi ya Everton, hatimaye kocha wa Manchester United, Jose Mourinho ametoa ufafanuzi kwanini alifanya maamuzi ya kumuingiza Marouane Fellain katika mchezo wa jana na baadae kusababisha penalti, anaandika Kelvin Mwaipungu.

“Everton si timu ya kutoa pasi kama walivyokuwa zamani. Everton ya sasa ni klabu inayocheza moja kwa moja, Ashley Williams moja kwa moja, Ramiro Funes Mori moja kwa moja. Kila kitu moja kwa moja.

“Unapokuwa na mchezaji wa kimo cha mita mbili kwenye benchi unamchezesha kwenye safu ya ulinzi kuisaidia timu kushinda mipira,” amesema Mourinho.

Hii ni mara ya pili kwa mchezaji huyo kufanyiwa mabadiliko huku timu ikiwa inaongoza na baadae mchezo kumalizika kwa sare, huu unaweza kuwa msimu mbaya kwa mchezaji huyo ambaye ni msimu wake wa tatu toka alipojiunga na klabu hiyo kutokea Everton.

Manchester United inapata sare ya tatu mfululizo katika michezo ya ligi hiyo na kufikisha jumla ya pointi 21 na ikishika nafasi ya sita huku ikiwa nyuma kwa pointi 13 kutoka kwa Chelsea ambayo ni vinara wa ligi hiyo kwa sasa baada ya kuchezwa michezo 14.

error: Content is protected !!