September 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Urais Z’bar: CCM yampitisha Dk. Mwinyi

Dk. Hussein Mwinyi, Mgomnbea Urais Zanzibar (CCM)

Spread the love

DAKTARI Hussein Ali Mwinyi amechaguliwa kwa asilimia 78 za wajumbe wa Halmashauri Mkuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwa mgombea urais wa Zanzibar katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2020. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Akitangaza matokeo hayo, Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai amesemaq, Dk. Mwinyi amepata kura 129 sawa na asilimia 78.65, Shamsi Vuai Nahidha kura 16 na Dk. Khalid Salum Muhamed kura 19.

Katika uchaguzi huo, Dk. Mwinyi atashiriki uchaguzi huo kumrithi Rais Ali Mohamed Shein ambaye hatogombea kutokana na kumaliza muda wake wa miaka kumi ya uongozi.

Endelea kufuatilia MwanaHALISI Online na MwanaHALISI TV kwa habari zaidi

error: Content is protected !!