Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Urais NCCR-Mageuzi: Aboubakar achukua fomu, asema ndoto yake imetimia
Habari za Siasa

Urais NCCR-Mageuzi: Aboubakar achukua fomu, asema ndoto yake imetimia

Spread the love

ABOUBAKAR Juma Aboubakar leo Jumamosi tarehe 18 Julai 2020 amechukua fomu kuomba ridhaa ya Chama cha NCCR-Mageuzi, kugombea Urais wa Tanzania, katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2020. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam.

Aboubakar amekabidhiwa fomu hiyo na Anthony Komu, Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya NCCR-Mageuzi, kwenye Ofisi za Makao Makuu ya chama hicho, Ilala jijini Dar es Salaam.

Baada ya kukabidhiwa fomu hiyo, Aboubakar amesema, ameamua kutia nia kugombea nafasi hiyo, ili apate fursa ya kuwaongoza Watanzania, katika misingi ya utu, maadili, umoja na udugu kama itikadi ya NCCR-Mageuzi inavyoelekeza.

Mwanasiasa huyo amesema, safari ya kusaka nafasi ya kugomnea Urais wa Tanzania aliianza miaka 28 iliyopita, hivyo anaamini NCCR-Mageuzi kitakamilisha safari yake hiyo kwa kumpitisha kuwa mgombea wake.

“Niliianza safari hii kwa muda wa miaka 28, kila siku nilikua msindikizaji. Lakini leo natia nia kugombea urais wa Tanzania ili niwe mtumishi wa Watanzania wote bara na Zanzibar na wa rika zote,” amesema Aboubakar.
Amesema yeye ni Mtanzania mwenye asili ya Zanzibar aliyezaliwa Lushoto Mkoa wa Tanga na makazi yake yote yapo Ilala jijini Dar es Salaam.

Aboubakar amesema anaona Katiba ya Tanzania inamsuta “na nimeifanyia nini Tanzania wakati nikiona wengine wametupwa nje ya mfumo wa kijamii, kisiasa na kielimu” nah ii ndiyo imenisukuma kujitokeza kuwania uongozi huu.

Naye Komu amesema, chama hicho kiko tayari kutoa ushirikiano kama atafanikiwa kushinda mchakato wa uteuzi ndani ya NCCR-Mageuzi.

“Mimi kama mwenyekiti, nimwambie sisi tuko tayari kukuunga mkono kwenye nia yako nzuri na kukupa kila aina ya ushirikiano katika kufanikisha nia hii nzuri, na hiyo itakua kamili zaidi utakapofanikiwa kuwa mgombea kwa tiketi ya chama chetu kama ukijaaliwa,” amesema Komu.

Mwenyekiti huyo wa Uchaguzi NCCR-Mageuzi, amemtaka mti ni huyo kusoma vyema katiba ya chama hicho, ili imuongoze katika harakati zake hizo.

“Uchaguzi ni jambo kubwa linaweza amua mustakabali wa maisha yetu au iendelee kuwa na amani na utulivu tunaoupenda au tuingie kwenye historia nyingine ya mfarakano, nikuombe sana chama chetu kina itikadi, tuna katiba, kanuni na mambo mengine,” amesema Komu na kuongeza.

“Itikadi yetu ni ya utu kwa mujibu wa katiba ya chama inasema, itikadi ya chama ni utu ambayo msingi yake undugu, maadili, usawa, haki, imani, mabadiliko, uhuru, wajibu, asili, kazi na endelezo. Hizi ni dhana pana sana, sasa wajibu wetu kujifunza na kuzielewa kisha kuzitekeleza,” amesema

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!