January 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Urais CCM kumekucha, wanne waingia mitini na fomu

Katibu wa Halmashauri kuu ya CCM Idara ya Oganezesheni Dr Mohamed Seif Khatibu akizungumza na Waandishi wa Habari makao makuu Dodoma kuhushu ratiba ya uchukuaji na urudishaji fomu

Spread the love

PAZIA la uchukuaji na urejeshaji wa fomu za kuomba kuteuliwa kuwania nafasi ya urais ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM), limefungwa rasmi jana jioni. Anaandika Dany Tibason … (endelea). 

Mpaka pazia hilo limefungwa watia nia wanne kati ya 42 walishindwa kurejesha fomu licha ya kulipia ada ya Sh. milioni moja ya kuomba uteuzi wa kurithi kiti cha rais Jakaya Kikwete anayemaliza muda wake Oktoba mwaka huu. 

Kufungwa kwa pazia hilo kutoa nafasi sasa ya chama hicho tawala nchini kuingia katika hatua nyingine ngumu zaidi ya kufanya uteuzi wa nani anayefaa miongoni mwao kupeperusha bendera ya CCM.

Tayari presha ya vikao hivyo vinavyotarajiwa kuanza wiki ijayo iko juu na baadhi ya wagombea na wapambe wao wako mjini hapa kwa ajili ya kufanya harakati za mwisho za kuomba kuteuliwa.

Luhavi atangaza kufunga pazia

Akitangaza kufunga pazia hilo, Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, Rajabu Ruhavi alisema kuwa zoezi hilo limefungwa rasmi jana huku wagombea wanne wakishindwa kurejesha fomu zao..

Alisema kuwa zoezi hilo lililoanza Juni tatu mwaka huu lilifanyika kwa utulivu na jumla ya wagombea 42 walichukuwa fomu na waliofanikiwa kurudisha fumu hizo ni wagombea 38 ambao walikamilisha masharti ya chama kwa kutafuta wadhamini katika mikoa 15 na kati ya hiyo, ikiwemo mikoa mitatu  ya Zanzibar.

Aidha Luhavi aliwataja walioshindwa kurudisha fomu ni Dk, Mussa Kolokola, Peter Nyalali, Helena Eliniwenga na Antony Chalamila.

Hata hivyo Luhavi alisema mgombea mmoja aliyejulikana kwa jina la Helena Eliniwenga alizitelekeza fomu hizo katika moja ya ofisi za makao makuu ya chama siku aliyokuja kuchukua baada ya kulipia ada.

“Eliniwinga baada ya kuchukuwa fomu aliingia katika moja ya ofisi za makao makuu ya chama na kuhitaji kupewa elimu ya siasa na utaratibu wa kupata wadhamini na alipoambiwa muda huo sio muafaka, alizitelekeza na kuondoka,” amesema Luhavi.

Waliochukua na kurejesha fomu hizo ni Samuel Sitta, Dk. Ghalib Bilal, Dk. Asha Rose Migiro, Amos Siyantema, Malick Maruku, Agustino Mahiga, Makongoro Nyerere, Profesa Mark Mwandosya, Balozi Sefu Karume, John Magufuli, Boniface Ndengo, Mathias Chikawe, Titus Kamani, Steven Wasira, Sospeter Muhongo, Leonce Mulenda na Jaji Augustine Ramadhani.

Wengine ni Benard Membe, Frederick Sumaye, Balozi Amina Salumu Ally, Mizengo Pinda, Harrison Mwakyembe, Mwele Malechela, Joseph Chaggama, Mwigulu Nchemba, Lazaro Nyalandu, Dk, Hamis Kigwangwala, Dk. Hassy Kitine, Luhaga Mpina, Eldfonce Bihole, Edward Lowassa, William Ngereja, January Makamba, Balozi Patrick Chokala, Mwalimu Banda Sonoko, Godwin Mwapongo na Rita Ngowi

error: Content is protected !!