April 18, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Uporaji nyumbani kwa Dk. Mengi

Spread the love

WATU ambao hawajatambulika, wamepora vito vya thamani wakati wa shughuli ya maziko ya mfanyabiashara na aliyekuwa mkurugenzi wa kampuni zilizo chini ya IPP Group, Dk. Reginald Abraham Mengi. Anaripoti Mwandishi Maalum, Machame … (endelea).

Taarifa kutoka ndani ya familia hiyo zinaleza kuwa, vito hivyo viliporwa wakati wa shughuli ya mazishi ya Dk. Mengi, yaliyofanyika nyumbani kwake Nkuu, Machame katika Jimbo la Hai mkoani Kilimanjaro.

Vito vinavyotajwa kuporwa ni pamoja na mikufu ya dhahabu, kompyuta mpakato pamoja na fedha ambazo kiasi chake hakijatajwa.

Benson Mengi, msemaji wa familia hiyo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, hata hivyo ameeleza kuwa, uchunguzi unaendelea kufanywa na Jeshi la Polisi ili kubaini aliyehusika.

Vitu vyote hivyo imeelezwa vilikuwa kwenye jumba la kifahali la Dk. Mengi na mkewe Jacqueline Mengi, mahala ambapo amezikwa mfanyabiashara huyo Alhamisi wiki hii.

Taarifa zaidi zinaeleza kuwa, wakati wa msiba kulikuwepo na watu wengi ambao miongoni mwao wanadaiwa kujieleza ni sehemu ya familia hiyo.

Na kwamba, kutokana na mazingira yalivyokuwa, ilikuwa ni vigumu kutambuana wote jambo ambalo lilitoa mwanya kwa watu kuingia hata maeneo wasiyoruhusiwa.

Hamis Issah, Kamanda wa Polisi Mkoa Kilimanjaro amesema, polisi wameanza uchunguzi juu ya tukio hilo na kwamba, mpaka sasa wanashikilia watu wawili.

Hata hivyo ameeleza kuwa, uchunguzi zaidi unaendelea na kwamba, kwenye uchunguzi huo, baadhi ya watu wameeleza kuwa, miongoni kwa wawashukiwa walikuwa wamevaa vitambulisho vilivyoandika IPP.

“Kenye familia ile, kulikuwa na watu wengi hawajuani,” amesema Kamanda Issah na kuongeza, “jambo hilo limesababisha kila mtu kuingia mahali hata asiporuhusiwa.”

Dk. Mengi (77) alifariki dunia tarehe 2 Mei 2019 alipokuwa Dubai, Falme za Kiarabu na kuzikwa kijijini kwao Nkuu, Machame mkoani Kilimanjaro.

error: Content is protected !!