Friday , 1 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Upinzani wazidi kubomoka, Mbunge wa CUF arudi CCM
Habari za SiasaTangulizi

Upinzani wazidi kubomoka, Mbunge wa CUF arudi CCM

Spread the love

MAULID Mtulia, Mbunge wa Kinondoni kwa tiketi ya Chama cha Wananchi CUF amejiuzulu uanachama na ubunge kupitia chama hicho kwa madai kuunga mkono juhudi za Rais John Magufuli, anaandika Faki Sosi.

Mtulia amesema amefikia uamuzi huo kwa kuwa mambo yote waliyoahidi tayari yanafanywa vizuri zaidi na CCM hivyo ni vigumu kuwa mpinzani.

Aidha ametanabaisha kuwa kwa sasa ili uwawakilishe wananchi vizuri inabidi uwe CCM kwani ndo kuna sera za kusaidia wananchi kwa sasa. Hivyo imekuwa ikimuwia vigumu kufanya kazi akiwa nje ya CCM.

Mbunge huyo amesema kwa hiari yangu ameamua kujiuzulu uanachama wa CUF na kujiuzulu nafasi zake zote za uongozi nilizokuwa nashikilia kuanzia Desemba 2, 2017.

* Upinzani kupata pigo

Amesema s​ababu za kuchukua uamuzi huo ni kutokana na uzoefu alioupata kwa miaka miwili ya ubunge ambapo amebaini kuwa Serikali ya CCM inafanya kazi kubwa ya kutekeleza Ilani na imefanya vizuri katika mambo mengi ambayo upinzani waliahidi kuyatekeleza.

Hivyo haoni sababu ya kuendelea kuwa upinzani na badala yake ameona ni vema aungane na juhudi za Serikali kwa kumuunga mkono Rais Magufuli katika kuwaletea wananchi maendeleo na kukabiliana na kero mbalimbali.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Mwili wa Hayati Mwinyi kuagwa leo saa 8 Uwanja wa Uhuru

Spread the loveMWILI wa Rais Mstaafu, Ali Hassan Mwinyi unatarajiwa kuagwa kuanza...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Mwinyi kuzikwa Machi 2 visiwani Unguja

Spread the loveMWILI wa aliyekuwa Rais wa Awamu ya Pili wa Tanzania,...

Habari za SiasaTangulizi

Rais mstaafu Mwinyi afariki dunia

Spread the loveRais Mstaafu wa awamu ya pili wa Tanzania, Ally Hassan...

Habari za Siasa

Waziri mkuu Ethiopia atua Tanzania

Spread the loveWaziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Shirikisho la Ethiopia,...

error: Content is protected !!