Wednesday , 29 March 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Upinzani wapoteza vigogo hawa bungeni  
Habari za SiasaTangulizi

Upinzani wapoteza vigogo hawa bungeni  

Joseph Haule
Spread the love

TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) nchini Tanzania kimeendelea kutangaza matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa madiwani, wabunge na Urais uliofanyika jana Jumatano tarehe 28 Oktoba 2020. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Matokeo hayo yanaonyesha Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinaongoza kwa mbali kwa nafasi zote za udiwani, ubunge na Urais ambapo mgombea wake, Rais John Magufuli anawaongoza wenzake.

Pia, matokeo yanaonyesha vigogo wa upinzani wakiongozwa na aliyekuwa kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani bungeni nchini Tanzania, Freeman Mbowe akitangazwa kushindwa Jimbo la Hai Mkoa wa Kilimanjaro.

Kinachoendelea kuonekana ni tofauti na Uchaguzi Mkuu uliopita mwaka 2015, kati ya majimbo 264 ya uchaguzi, vyama vya upinzani kwa pamoja vilipata majimbo 69 huku CCM ikijikusanyika majimbo 195.

Mpaka inafika 12 jioni jioni, kati ya majimbo 264 ya uchaguzi, CCM imejikusanyia zaidi ya majimbo 128 na kupoteza moja la Mtwara Vijijini lililokuwa likiongozwa na Hawa Ghasia.

Ghasia ametangazwa kushindwa na Shamsia Mtamba wa CUF aliyepata kura 26,262 huku Ghasia aliyewahi kuwa waziri katika utawala wa Rais mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete akipata kura 18,505.

Jimbo ha Hai, Mbowe ameshindwa na Shaashisha Mafuwe wa CCM aliyepata kura 89,786 huku Mbowe akipata kura 27,684.

Freeman Mbowe

Mbowe ambaye ni Mwenyekiti wa kilichokuwa chama kikuu cha upinzani Tanzania, Chadema alikuwa akitafuta uongozi wa Jimbo la Hai kwa kipindi cha tatu mfululizo tangu alipoanza kuongoza mwaka 2010.

Hata hivyo, Mbowe aliongoza kwa mara ya kwanza Jimbo la Hai mwaka 2000 hadi 2005. Katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005, Mbowe aligombea Urais na kushindwa na Jakaya Mrisho Kikwete wa CCM.

Mwaka 2010, Mbowe alirejea jimboni na wananchi walimchagua kuwaongoza.

Mbali na Mbowe, wabunge wengine wa Chadema walioangushwa kwenye uchaguzi huo ni; Joseph Mbilinyi maarufu Sugu wa Mbeya Mjini aliyeongoza jimbo hilo kwa miaka kumi mfululizo  ameshindwa na Dk. Tulia Ackson wa CCM.

Mch. Peter Msigwa

Mchungaji Peter Msigwa aliyekuwa anaongoza Jimbo la Iringa Mjini kwa miaka kumi mfululizio, katika uchaguzi mkuu mwkaa huu, ameshindwa na Jesca Msambatavangu wa CCM.

Tarime Vijiji, kumeshuhudiwa John Heche aliyeongoza jimbo hilo kwa msimu mmoja tangu lilipoanzishwa mwaka 2015 akitangazwa kushindwa na Mwita Waitara wa CCM.

Joseph Haule maarufu Profesa J, ametangazwa kushindwa kutetena Jimbo la Mikumi aliyeliongoza kwa miaka mitano pekee mwaka 2015-2020 na mgombea wa CCM, Dennis Londo.

Salome Makamba

Bunda Mjini lililokuwa likiongozwa na Ester Bulaya, ametangazwa kushindwa na Robert Maboto wa CCM.

Bulaya aliingia bungeni kwa mara ya kwanza mwaka 2010 akiwa mbunge wa Viti Maalum kupitia CCM, katika uchaguzi mkuu mwaka 2015 aligombea Bunda Mjini kupitia Chadema na kumshinda Steven Wassira wa CCM.

Jimbo la Tarime Mjini lililokuwa likiongozwa na Esther Matiko, naye ameshindwa kutetea jimbo hilo na kujikuta akilipoteza kwa Michael Kembaki wa CCM huku Catherine Ruge aliyejitosa jimboni kwa mara ya kwanza Serengeti akishindwa na Amsabi Mrimi wa CCM.

Frank Mwakajoka

Frank Mwakajoka amejikuta akishindwa na David Silinde wa CCM jimbo la Tunduma.

Silinde amekuwa mbunge kwa miaka kumi kupitia Chadema na mwaka huu, alihamia CCM ambako ameendelea kupata ridhaa ya wananchi kuwatumikia.

Shinyanga Mjini, kama kulivyo katika majimbo mbalimbali nchini, Salome Makamba ametangazwa kushindwa na Patrobas Katambi wa CCM.

Upendo Peneza aliyekuwa mbunge wa viti maalum ambaye mwaka huu alijitosa jimbo la Geita Mjini, ameshindwa na Constantine Kanyasu wa CCM.

Ester Bulaya

Kigoma Mjini, imeshuhudia Zitto Kabwe wa ACT-Wazalendo akitangazwa kushindwa kwa kupata kura 20,600 huku Kirumbe Ng’enda wa CCM aluyeibuka mshindi akipata kura 27,638.

Zitto ambaye ni Kiongozi wa ACT-Wazalendo aliingia bungeni kwa mara ya kwanza mwaka 2005 kupitia Chadema katika Jimbo la Kigoma Kaskazini aliloliongoza kwa miaka kumi mfululizo na mwaka 2015 aligombea Kigoma Mjini kupitia ACT-Wazalendo na kuibuka mshindi.

Zitto Kabwe

Endelea kufuatilia MwanaHALISI Online, MwanaHALISI TV na mitandao yetu ya kijamii kwa habari na taarifa mbalimbali.

2 Comments

  • CHADEMA mukubali matokeo, rais Magufuli na CCM wamewatumikia watanzania ki haki, yoote inaonekana ulimwenguni koote.
    Mataifa ya mabeberu wana wivu ya inchi yenu, hawataki kiongozi wa kuleta maendeleo kama Magufuli.
    Nawaomba CHADEMA mujifunze kusema kweli, na siyo kutusi wagombea wengine. TUNDU LISSU njoo chanjo cha maanguko yenu nyoote nyinyi CHADEMA, LISSU hafai kwenye siasa kabisa

  • Sikutarajia lisu angekuja na ajenda za ajabu zisizo mgusa mwsnanchi wa kawaida wakulaumiwa ni lisu lakn pia kama chama hawakujipanga mapema na kutafuta mgombea mahiri wa kupambana na mh Magufuri kiongozi huyo kwa aliyolifanyia Taifa alistahli kupewa kura za kutosha hongera CCM kwa ushindi mnono mlioupata msibweteke kwa ushindi hupo chapeni kazi cc wanachi tunasubili maendereo tuu,

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

TEMESA iliyokarabati Kivuko kwa Bil 7.5 yapata hati chafu

Spread the love  MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),...

Habari za Siasa

ACT-Wazalendo yakusanya Mil 8.5/- kodi ya zuio na kutokomea nazo

Spread the love  MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),...

Habari za Siasa

DC Kasilda Mgeni ahamasisha chakula shuleni

Spread the love  MKUU wa Wilaya ya Same, mkoani Kilimanjaro, Kasilda Mgeni...

Habari za Siasa

Bilioni 223.9 zapelekwa Tunduru ndani ya miaka 2 ya SSH

Spread the love  ZAIDI ya Sh. bilioni 223.9 zimepelekwa Wilaya ya Tunduru...

error: Content is protected !!