August 8, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Upinzani wapeta Ghana

Nana Akufo Addo

Spread the love

NANA Akufo Addo, kiongozi wa chama cha upinzani cha New Patriotic Party (NPP) anaongoza katika matokeo ya uchaguzi mkuu uliofanyika wiki iliyopita nchini Ghana, anaandika Wolfram Mwalongo.

Addo yupo mbele ya mpinzani wake John Mahama ambaye ndiye aliyepo madarakani kwa kura asilimia 54 huku mpinzani wake (Mahama) akiwa na asilimia 44 ya kura.

Rais Mahama amedhihirisha kwamba atapokea matokeo yoyote yatakayotangazwa mara tu baada ya Tume ya Uchaguzi nchini humo kufanya hivyo.

Hata hivyo, Addo amewataka wafuasi wake na wanachama wa NPP kuwa watulivu wakati wakisubiri Tume ya Uchaguzi kutangaza matokeo na kuwa, ushindi huo ni wa kihistoria katika taifa hilo.

“Chama chetu cha NPP kimekuwa kimya kutokana na imani kubwa ya ushindi tulioupata kwasababu ni wa kihistoria katika taifa letu,” amesema.

Ingawa hivi sasa taarifa kutoka nchini humo zinasema kwamba, chama kilichopo cha National Democratic Congress (NDC) kinachoongozwa na Rais Mahama kimepinga matokeo hayo huku kikitaka uchaguzi urudiwe.
Koku Anyidoho, kiongozi wangazi ya juu wa NDC amesema, chama chao ndio kinachoongoza uchaguzi huo.
Anyidoho amesai kwamba, Chama cha NPP kimefanya hila za uvuruga uchaguzi huo, “tumefanya uchambuzi wa kina, tumegundua Rais Mahama ndiye anayeongoza,” amesema katika mkutano wake na waandishi wa habari leo asubuhi.

error: Content is protected !!