Saturday , 20 April 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Upinzani wamkaba koo Rais Ufaransa, uchaguzi waingia duru ya pili
Kimataifa

Upinzani wamkaba koo Rais Ufaransa, uchaguzi waingia duru ya pili

Spread the love

RAIS wa Ufaransa, Emmanuel Macron na kiongozi wa mrengo wa kulia Marine Le Pen wanatarajiwa kuingia katika duru ya pili ya uchaguzi mkuu nchini humo tarehe 24 Aprili mwaka huu baada ya kushindwa kufikia asilimia 50 ya kura katika uchaguzi uliofanyika jana tarehe 10 Aprili mwaka huu. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea)

Katika duru hiyo ya kwanza ya uchaguzi wa rais, mgombea urais kwa chama cha Rassemblement National, Marine Le Pen aliyepata alipata asilimia 23.3 wakati rais anayemaliza muda wake Emmanuel Macron kutoka chama cha La République en Marche ambaye amepata asilimia 28.1.

Katika uchaguzi huo ambao Ufaransa inatajwa kuwa na wapiga kura milioni 48, ulihusisha wagombea 12 wa kiti cha Urais.

Kando na wagombea wakuu hao wawili, mgombea mwengine wa siasa kali za mrengo wa kushoto Jean-Luc Melenchon ni miongoni mwa watu mashuhuri wanaowania kuingia Ikulu ya rais ya Elysée.

Kwa matokeo hayo Rais anayeondoka Emmanuel Macron na mgombea wa RN, Marine Le Pen wamejipatia nafasi ya kuingia katika duru ya pili baada ya kupata kura zinazohitajika kuingiakatika duru ya pili itakayofayika mnamo Aprili 24.

Kutokana taratibu za uchaguzi nchini humo, hakuna mshindi aliyepatikana katika duru ya kwanza ya uchaguzi kwani mshindi alitakiwa kupata asilimia 50 za kura zote zilizohesabiwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Kimataifa

Majaji kuamua hatima ya Zuma leo

Spread the loveMajaji nchini Afrika Kusini leo Jumanne wataamua ikiwa rais wa...

Habari za SiasaKimataifa

Spika Afrika Kusini ajiuzulu kwa tuhuma za rushwa

Spread the loveSpika wa Bunge la Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa-Nqakula ametangaza kujiuzulu...

Habari MchanganyikoKimataifa

Tetemeko la ardhi laua 7, lajeruhi 800 Taiwan

Spread the loveWatu wapatao saba wamefariki dunia na wengine zaidi ya 800...

error: Content is protected !!