January 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Upinzani waleta neema kwa Polisi

Spread the love

UPINZANI anaotoa Mgombea wa Urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) anayeungwa mkono na vyama vinavyounda umoja wa Katiba ya Wananchi, (Ukawa) Edward Lowassa umeleta neema kwa makundi ambayo yalisahauliwa siku nyingi wakiwemo Askari. Anaandika Josephat Isango … (endelea).

“Ni kweli tumeongezewa resheni (pesa ya kujikimu toka 180,000 hadi 300,000 mwezi huu, wanaopokea mishahara toka CRDB walipata kati ya Oktoba 8 na 9 lakini sisi wa NMB tumepokea baada ya tarehe hizo”.

Akizungumza na Mwanahalisi Online, askari mmoja ambaye hakupenda kutajwa jina lake, alithibitisha kuwa sasa serikali imewaongezea hela hizo, na wanawashukuru viongozi wa kambi ya upinzani waliopigania kudai askari waongezewe posho hizo

“Sisi tunawashukuru wapinzani maana wamekuwa wakitutetea usiku na mchana, sasa naona wamesikia na wametuongezea nadhani hapa ni baada ya kugundua kuwa wamebanwa na wapinzani kwenye kampeni.

Akizungumza Bungeni kwa niaba ya Kambi rasmi ya Upinzani, Waziri wa kivuli wa Mambo ya ndani na Mbunge wa Arusha Godbless Lema alisema , “kufuatia ugumu wa maisha ya Askari wetu wa Jeshi la Polisi, Kambi Rasmi yaUpinzani Bungeni, kwa miaka yote ya utawala wa Serikali ya awamu ya nne, imekuwa ikiitaka Serikali, kuongeza posho ya chakula (Ration allowance) kwa askari wa Jeshi la Polisi iliwalau posho hiyo ishabihiane na posho ya Jeshi la Wananchi waTanzania (JWTZ) ili waweze kukabiliana na ugumu wamaisha.

Kwa mujibu wa kumbukumbu rasmi za bunge (hansard) Waziri waFedha wa wakati huo Marehemu William Mgimwa alikubali posho yachakula ya shilingi 225,000/= kwa mwezi sawa na shilingi 7,500/= kwasiku kwa kila askari. Taarifa tulizo nazo ni kwamba posho hiyohaijalipwa mpaka leo, licha ya Serikali kuahidi kuwalipa posho hiyo.

MheshimiwaSpika,katika mazingira kama haya ambapo Serikali inaahidi ndani ya Bunge hili kupandisha posho za chakula za askari Polisi halafuhaitekelezi, inataka tuishauri nini tena?

MheshimiwaSpika,kwa kuwa hoja ya kupandisha “rationallowance”kwa askari wetu wa Jeshi la Polisi ilianzishwa na Kambi ya Upinzani,na kwa kuwa kwa miaka yote ya utawala wa Serikali ya awamu ya nne Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni imekuwa ikiwatetea askari waJeshi la Polisi ili walipwe posho ya chakula ya shilingi 7,500/= kwa siku kwa kila askari; na kwa kuwa kwa mihula yote miwili ya utawalawa Serikali ya awamu ya nne.

Serikali imeshindwa kutekeleza ahadi yake yenyewe iliyoitoa hapa Bungeni kwamba ingepandisha posho hiyo,hivyo basi Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inapenda kuchukua nafasi hii kuwaahidi Askari wote waliopo chini ya Jeshi la Polisi kwamba endapo Upinzani utaunda Serikali baada ya ushindi katika uchaguzimkuu wa Oktoba, 2015, posho hiyo itapandishwa haraka iwezekanavyokwa kuwa ni sera ya Upinzani kuboresha maslahi ya askariwa Jeshi la Polisi.

Ili kutimiza azma hiyo, Kambi Rasmi yaUpinzani Bungeni inalitaka Jeshi la Polisi Nchini kukataa kutumika kiasiasa na Serikali ya CCM kuukandamiza upinzani na badala yakewafanye kwazi kwa kuzingatia sheria na taratibu zinazotumika kuongozautendaji wa Jeshi hilo.

Uchunguzi uliofanywa na MwanaHalisi umebaini kuwa wiki hii kundi jingine ambalo linatarajiwa kukumbukwa ni la Waalimu ambao wamekuwa wakiidai serikali madeni makubwa.

error: Content is protected !!