Friday , 1 March 2024
Habari za SiasaTangulizi

Upinzani kupata pigo

Maalim Seif Sharif Hamad, aliyekuwa Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar (2010-2015) (wakwanza) akiteta jambo na Waziri mkuu mstaafu Edward Lowassa
Spread the love

WABUNGE wawili kutoka vyama vya CUF na Chadema, wako mbioni kuvihama vyama vyao, imeelezwa, anaandika Mwandishi Wetu.

Taarifa kutoka kwa watu waliokaribu na wabunge hao zinasema, kumekuwa na vikao mfululizo kati ya viongozi wa Chama Cha Mapinduzi na serikali yenye lengo la kuwashawishi wawakilishi hao wa wananchi.

Kwa mujibu wa habari hizo, mikakati ya kuondoka kwa wabunge hao inaratibiwa na mmoja wa viongozi wa ngazi ya juu wa CCM jina tunalihifadhi.

Chanzo cha kuondoka kwa wabunge hao kimetajwa kuwa ni kutoelewana na baadhi ya viongozi wao ndani ya vyama hivyo.

“Huyu mmoja amechoshwa na uongozi wa mwenyekiti wake Freeman Mbowe, wakati huyu mwingine amechoshwa na mgogoro ndani ya chama chake cha CUF,” ameeleza mmoja wa marafiki wa karibu wa wabunge hao.

Anasema, “Yule mwingine analalamika kusakamwa na kubaguliwa, kutokana na kutofautiana na kiongozi mkuu wa chaama. Hivyo ameamua kuondoka ili kulinda hadhi na heshima yake.”

Wabunge wote wawili, wameingia bungeni kupitia majimbo ya uchaguzi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Mwili wa Hayati Mwinyi kuagwa leo saa 8 Uwanja wa Uhuru

Spread the loveMWILI wa Rais Mstaafu, Ali Hassan Mwinyi unatarajiwa kuagwa kuanza...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Mwinyi kuzikwa Machi 2 visiwani Unguja

Spread the loveMWILI wa aliyekuwa Rais wa Awamu ya Pili wa Tanzania,...

Habari za SiasaTangulizi

Rais mstaafu Mwinyi afariki dunia

Spread the loveRais Mstaafu wa awamu ya pili wa Tanzania, Ally Hassan...

Habari za Siasa

Waziri mkuu Ethiopia atua Tanzania

Spread the loveWaziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Shirikisho la Ethiopia,...

error: Content is protected !!