July 1, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Upigaji kura Uganda wayumba

Spread the love

WAPIGA kura nchini Uganda wanaendelea kupiga kura vituoni kuwachagua viongozi lakini katika baadhi ya vituo upigaji kura umeyumba kutokana na kuchelewa kuanza.

Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) limeripoti kwamba, hali hiyo imetokana na vifaa na karatasi za kupigia kura kutofikishwa vituo kwa wakati katika baadhi ya maeneo.

Mjini Kampala ambapo ni Makao Makuu ya Tume ya Uchaguzi nchini humo, bado kuna vituo ambavyo kufikia saa nne upigaji kura haukuwa umeanza.

Hata hivyo, tume hiyo kwenye ukurasa wake wa Twitter, imeandika: “Tunabaki kuwa na matumaini na tunawahikishia kwamba nyote mtaweza kupiga kura leo. Tunasikitika kutokana na kuchelewa huku. Asanteni.”

Kuhusu iwapo muda wa kupiga kura utaongezwa, tume hiyo kupitia mitandao ya kijamii imesema kwa mujibu wa sheria, ni sharti vituo vifungwe saa kumi alasiri.

Tume hiyo imeahidi kuhakikisha wapiga kura wote watakaojitokeza kufikia wakati huo wanapiga kura.

error: Content is protected !!