March 9, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Upepo mkali waleta maafa Mafia

Spread the love

UPEPO unaoendelea kuvuma kwenye Ukanda wa Pwani umesababisha kifo cha mtu mmoja aliyedondokewa na mnazi kisiwani Mafia. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Mtu huyu aliyefahamika kwa jina la Mwandeta Juma aliangukiwa na mnazi uliodondoka kutokana na upepo mkali unaovuma katika Kijiji cha Futa Luma, Tarafa ya Kaskazini mwa Mafia.

Mwandeta mwenye umri wa miaka 11 amefariki papo hapo kutokana na kudondokewa na mnaza huo jana tarehe 23 Oktoba mwaka 2018 na kuzikwa leo.

Tarehe 19 Oktoba mwaka huu Mamlaka ya Hali ya Hewa ilitoa tahadhari ya upepo mkali sambamba na mawimbi makubwa baharini katika maeneo mbalimbali nchini. Kutokana upepo huo, usafiri wa bahari umezuiwa mpaka hali ya hewa itakapokuwa shwari.

error: Content is protected !!