August 10, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Upelelezi wa Lowassa bado pasua kichwa

Edward Lowassa alipowasili Makao Makuu wa Jeshi la Polisi

Spread the love

JESHI la Polisi Tanzania bado halijakamilisha upelelezi wa tuhuma zinazomkabiri Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, hivyo wamelazimika kumwachia na kumtaka arudi tena baada ya wiki tatu, anaandika Mwandishi Wetu.

Lowassa aliwasili Makao Makuu ya Polisi saa mbili asubuhi kama alivyoagizwa wiki iliyopita na kuingia moja kwa moja kwenye ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Boaz.

Waziri Mkuu huyo wa zamani aliambatana na mkewe, Regina na mwanasheria wake, Peter Kibatala.

Muda mchache mara baada ya kuwasili, Lowassa alipewa maelekezo kuwa upelelezi haujakamilika hivyo aliruhusiwa kuondoka na kutakiwa kurudi tena kwa DCI baada ya wiki.

Leo ni mara ya nne kwa Lowassa kuripoti hapo akituhumiwa kutoa kauli za kichochezi wakati wa futari iliyoandaliwa Juni 23, na Mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara.

Katika futari hiyo, Lowassa anadaiwa kutoa maneno ya uchochezi kuhusu masheikh wa Taasisi ya Uamsho wanaoshikiliwa gerezani akidai utaratibu wa kisheria ufanyike ili waachiwe huru.

error: Content is protected !!