August 9, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Uongozi UDOM wafumuliwa

Chuo Kikuu cha Dodoma

Spread the love

UONGOZI wa Chuo Kikuu cha Dodoma umefuliwa baada ya Mkuu wa Chuo hicho, Dk. Stergomena Tax kuteua sura mpya katika nafasi za juu za uongozi wa chuo hicho. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Katika taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana tarehe 27 Julai, 2022 na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kupitia kwa Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Wizara hiyo, Silvia Lupembe imeeleza kuwa Dk. Tax ameteua makamu mkuu wa chuo na manaibu makamu mkuu wa chuo hicho cha Dodoma.

Dk. Tax ambaye pia ni Waziri wa Ulinzi, amemteua Profesa Lughano Jeremy Kusiluka kuwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (VC) akichukua nafasi ya Profesa Faustine Karrani Bee.

Kabla ya uteuzi huo Profesa Kusiluka alikuwa Maamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mzumbe.

Dk. Stergomena Tax, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa

Aidha, Dk. Tax amewateua Profesa Razak Bakari Lokina kuwa Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma (DVC-ARC) na Profesa Winiester Anderson Saria kuwa Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Utawala (DVC-PFA).

Kabla ya uteuzi huo Profesa Lokina alikuwa Kaimu Amidi wa Shule Kuu ya Uchumi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Profesa Sari alikuwa Amidi wa Shule kuu ya Biashhara ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Manaibu makamu mkuu hao wa chuo hicho, wamechukua nafasi za Profesa Alexanda Makulilo Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma na Prof Donald Mpanduji aliyekuwa Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Utawala.

error: Content is protected !!