Thursday , 30 March 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko Uongozi Soko la Karikaoo matatani, Samia aagiza uchunguzi
Habari MchanganyikoTangulizi

Uongozi Soko la Karikaoo matatani, Samia aagiza uchunguzi

Spread the love

 

RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amemuagiza Waziri Ofisi ya Rais-Tamisemi, Ummy Mwalimu, kuwasimamisha kazi viongozi wa Shirika la Masoko ya Kariakoo, ili kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazowakabili. Anaripoti Jemima Samwel, DMC…(endelea).

Rais Samia ametoa agizo hilo leo Jumanne, tarehe 1 Juni 2021, alipofanya ziara ya kushtukiza katika masoko hayo na kupokea malalamiko kutoka kwa baadhi ya wafanyabiashara, kuhusu changamoto zinazowakabili hasa Wamachinga.

Baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wafanyabishara hao, Rais Samia alisema Serikali yake inaenda kufanya tathimini upya juu ya utendaji wa masoko hayo, huku akiagiza vyombo vya dola vifanye uchunguzi.

“Niwaahidi kama Serikali tunaenda kukaa kufanya tahimini ya soko, lakini nimuagize waziri wa Tamisemi kusimamisha uongozi uliopo na vyombo vya Serikali vifanye uchunguzi kwanza, halafu tutakuja kutoa maamuzi,” amesema Rais Samia.

Rais Samia amesema, baada ya Serikali kufanya tathimini hiyo, itaamua kama masoko hayo yaongozwe na watu binafsi au Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam.

“Tutafanya tena tahimini ya uongozi wa soko na tuone kama hili soko lisimamiwe na uongozi wa soko, au jiji lichukue soko,” amesema Rais Samia.

Akizungumzia ziara yake hiyo, Rais Samia amesema hali ya masoko hayo hairidhishi, ikiwemo mpangilio holela wa vibanda vya wafanyabiasha, pamoja na uongozi wa soko kutowasaidia Wamachinga.

“Nimeona kwanza Serikali tusaidie kusimamia na kufanya tathimini ya uendeshaji soko lote, sababu hali niliyoona ndani lakini hata nje kwenye vibanda hairidhishi hata kidogo. Kwa ujumla hali iliyopo hapa haikuniridhisha na tunakwenda kuchukua hatua inayofaa,”amesema Rais Samia.

Rais Samia amesema “Tuliyoyaona ndani na nimeongea na wanawake wawili watatu, naona usaidizi wa wafanyabiashara wadogo haupo . Ila kuna utengenezaji faida kwa shirika labda, lakini mipango ya kuingiza bidhaa hayampi nafuu mfanyabiashara mdogo.”

Rais Samia amewahakikishia wafanyabaishara katika masoko hayo, kwamba Serikali yake kupitia Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, itapanga utaratibu mzuri wa wao kufanya biashara.

“Kwa wakati huu naomba muendelee na baishara kwa usalama bila vurugu, Serikali iko pamoja nanyi, lakini wakati Serikali inawabeba, nanyi jitahidi kufuata sheria na taratibu zinazowekwa katika maeneo mlipo,” amesema Rais Samia.

Tarehe 22 Mei mwaka huu, Ummy alifanya ziara kwenye masoko hayo, na kukutana na malalamiko juu ya viongozi wake, ikiwemo baadhi ya wafanyabiashara kuuziwa vizimba hadi Sh. 5 milioni kwa kimoja.

Pamoja na ubadhirifu wa fedha za ushuru zinazotolewa na wafanyabishara hao.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

NMB yakabidhi vifaa vya ujenzi, samani kwa shule ya msingi Sinyaulime, Chuo cha FDC Morogoro

Spread the loveBENKI ya NMB imekabidhi vifaa vya ujenzi kwa shule ya...

Habari Mchanganyiko

NMB Bonge la Mpango – ‘Moto Uleule’ yazinduliwa, Milioni 180…

Spread the loveMSIMU wa tatu wa Kampeni ya kuhamasisha utamaduni wa Kuweka...

Habari Mchanganyiko

Rais Samia awataka wahariri kufanya kazi bila uoga, upendeleo

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan amewataka wahariri wa vyombo...

Habari Mchanganyiko

STAMICO yasaini mkataba wa bilioni 55.2 kuchoronga miamba GGML

Spread the loveSHIRIKA la Madini la Taifa (STAMICO) limezidi kufanya vizuri katika...

error: Content is protected !!