Wednesday , 29 March 2023
Home Kitengo Maisha Afya Unicef yalilia maisha ya watoto waliozaliwa Mwaka Mpya
Afya

Unicef yalilia maisha ya watoto waliozaliwa Mwaka Mpya

Spread the love

IKIWA ndani ya mwaka mpya watoto 48,000 wamezaliwa Ukanda wa Afrika Mashariki na Kusini shirika la watoto duniani Unicef limezisihi nchi za ukanda huo kuhakikisha kuwa watoto wanaishi na kubaki salama, anaandika Faki Sosi.

Leila Pakkala, Mkurugenzi wa UNICEF Kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika amesema kuwa Unicef imeazimia ndani ya mwaka 2018 ni kumsaidia mtoto kubaki salama kuanzia siku anayozaliwa.

“Katika Mwaka huu Mpya, azimio la UNICEF ni kusaidia kumpa kila mtoto zaidi ya saa moja, zaidi ya siku moja, zaidi ya mwezi mmoja  zaidi ya kuishi.

“Tunatoa wito kwa serikali na washirika kuendeleza na kupanua juhudi zao ili kuokoa maisha ya mamilioni ya watoto kwa kuleta ufumbuzi uliothibitishwa na wenye gharama ndogo.” amessema Pakkala,

Kila siku ndani ya Mwaka 2016 inakadiriwa watoto 2600 waliozaliwa walipoteza maisha ndani ya masaa 24  baada ya kuzaliwa.

Mwaka 2017 kwa mujibu wa ripoti ya umoja wa mataifa watoto 90,000 walikufa nchini Ethiopia na watoto 46,000 walikufa nchini Tanzania na kupeleka nchi ya  Ethiopia kushika nafasi ya tano na Tanzania kushika nafasi ya tisa kwenye nchi kumi duniani zenye viwango vya juu vya vifo vya watoto wachanga duniani.

Asilimia 80 ya vifo vyote vya watoto hao, vilisababishwa na vyanzo vinavyozuilika na kutibika kama vile kuzaliwa njiti, matatizo wakati wa uzazi, maambukizi kama vile bakteria na homa ya mapafu.

UNICEF inasema kwamba watoto waliozaliwa Mashariki na Kusini mwa Afrika watakuwa sawa na asilimia 12 ya watoto wachanga wanaokadiriwa kufika 386,000 watakaozaliwa duniani kote katika Siku ya Mwaka Mpya.

Takribani asilimia 58 ya vizazi hivi vitatokea katika nchi tano katika kanda hii, huku idadi ya juu zaidi ya vizazi hivi katika Siku ya Mwaka Mpya ikikadiriwa kuwa,Ethiopia watoto 9,023, Tanzania watoto 5,995, Uganda watoto 4,953, Kenya watoto 4,237 na Angola watoto 3,417.

Katika miongo miwili iliyopita, kumekuwa na maendeleo makubwa duniani katika kuokoa maisha ya mtoto, ambapo idadi ya vifo vya watoto kabla ya kutimiza umri wa miaka mitano imepungua kwa nusu hadi kufikia milioni 5.6 katika mwaka 2016.

 Matokeo ya utekelezaji wa programu za afya kama vile utoaji wa mara kwa mara wa chanjo, nyongeza ya Vitamini A, kuzuia maambukizo ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto, na kuimarisha udhibiti magonjwa yanayowaandama zaidi watoto imepelekea watoto wenye miaka mitano kuwa na nafasi ya kuishi nchi Tanzania.

Maniza Zaman, Mwakilishi wa UNICEF nchini Tanzania amesema kuwa lengo la Unicef kuokoa maisha ya kila mtoto pamoja na kuweka jitihada na kumfikia kila mama na kila mtoto mchanga na kuwapa huduma bora ya afya.

Ameleza licha kuwepo kwa maendeleo hayo bado kunachangamoto ambazo ni kufariki kwa mtoto wa chini ya miaka mitano kila siku na kupelekea idadi kufiki watoto 270 kufariki kila siku.

Zaman amevitaja vyanzo hivyo ni pamoja na ugonjwa wa malaria, ugonjwa wa mapafu, na kuhara. “Asilimia 60 ya vifo hivi hutokea ndani ya mwaka wa kwanza wa kuzaliwa.

Kadhalika, mwezi wa kwanza wa kuzaliwa bado umeendelea kuwa na changamoto kubwa ambapo asilimia 37.3 ya vifo vya watoto wachanga wenye umri chini ya miaka mitano hutokea ndani ya mwezi wa kwanza wa kuzaliwa.”

Ameeleza kuwa mwezi Mwezi Februari, UNICEF imekusudia kuzindua kampeni ya ‘Every Child Alive’, yaani ‘Kila Mtoto Aishi’, ambayo ni kampeni ya duniani kote inayohimiza upatikanaji wa ufumbuzi wa matunzo ya gharama nafuu na bora ya afya kwa kila mama na mtoto mchanga.

Ufumbuzi huu ni pamoja na upatikanaji kwa uhakika wa maji safi na salama na umeme katika vituo vya afya, uwepo wa mhudumu wa afya mwenye mafunzo wakati wa mtoto kuzaliwa, kuzuia maambukizi katika kitovu, kunyonyesha mtoto ndani ya saa la kwanza mara baada ya kujifungua, mtoto kuwa karibu na mama yake kiasi cha kugusana, yaani mama kumkumbatia mtoto wake.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfyaHabari

Ugonjwa wa ajabu ulioua watano Bukoka ni Marburg

Spread the loveWAZIRI wa Afya, Ummy Mwalimu amesema ugonjwa wa ajabu uliosababisha...

AfyaHabariHabari

Ugonjwa wa ajabu wadaiwa kuua watano Kagera, Serikali yatoa tahadhari

Spread the loveJUMLA ya watu watano wanaidaiwa kufariki dunia  katika vijiji vya...

Afya

LHRC yapinga kufutwa Toto Afya: Ni ukiukaji wa sheria za watoto

Spread the love  KITUO cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimekosoa...

Afya

Manesi 7 mbaroni tuhuma za kuwauzia dawa wagonjwa usiku wa manane

Spread the love  JUMLA ya wauguzi/manesi saba wa Hospitali ya Manispaa ya...

error: Content is protected !!