November 30, 2022

Uhuru hauna Mipaka

UNHCR: Tanzania imefanikiwa kulinda amani

Spread the love

 

SHIRIKA la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), limesema Serikali ya Tanzania imefanikiwa kulinda amani yake licha ya kuzungukwa na nchi zenye wasiwasi wa amani. Anaripoti Mwandishi Wetu, Morogoro … (endelea).

Kauli hiyo imetolewa leo Jumatano, tarehe 23 Novemba 2022 na Afisa Muhifadhi Wakimbizi Mwandamizi kutoka UNHCR nchini Tanzania, Boniface Kinyanjui katika warsha ya wahariri wa vyombo vya habari, mkoani Morogoro.

“Amani haitoki juu kushuka chini, inalindwa na Serikali. Serikali ya Tanzania imefanikiwa katika hili, ni nchi ya amani lakini imezingirwa na nchi zenye wasiwasi was amani,” amesema Kinyanjui.

Kinyanjui amesema Tanzania ni miongoni mwa nchi chache zilizopokea wakimbizi kutoka katika mataifa mbalimbali.

Amesema UNCHRC inapenda kuona wakimbizi na watu wanaoomba hifadhi wanapewa nafasi ya kufanya shughuli za uzalishaji Mali ili waweze kujikimu.

Afisa Muhifadhi Wakimbizi Mwandamizi kutoka UNHCR nchini Tanzania, Boniface Kinyanjui

“Wakimbizi na watu wanaoomba hifadhi sio watu wanaopendwa sana katika nchi nyingi. Sisi tungepenxa kuona wakimbizi wakipewa nafasi ya kujimudu kimaisha katika uzalishaji Mali maana ni wanadamu kama wengine. Katika wakimbizi Kuna wataalamu wengi ambao wanaweza kuisaidia jamii,” amesema Kinyanjui.

Amesema, Kuna raia mmoja wa Sudan Kusini, alipita Tanzania kuelekea Afrika Kusini, ambaye alitengeneza mfumo was kuingiza hewa kwenye mwili kupitia tundu za pua wakati wa Ugonjwa wa Virusi vya Korona ulioibuka 2019 (UVIKO-19).

error: Content is protected !!