Friday , 29 September 2023
Home Kitengo Habari Kimataifa Undani wa kinachoendelea Zimbabwe huu hapa
Kimataifa

Undani wa kinachoendelea Zimbabwe huu hapa

Spread the love

KUMEKUWA na sintofahamu ya kile kinachoendelea nchini Zimbabwe huku kukiwa na taarifa tofauti ya mapinduzi yaliyofanyika nchini humo dhidi ya Rais Robert Mugabe na mgogoro ndani chama chake cha Zanu PF.

Hii hapa matukio yanaoendelea nchini humo na undani wa mgogoro huo

Magari ya kijeshi katika mitaa ya Harare

Magari ya kijeshi yanaonekana yakipiga doria katika barabara za mji mkuu wa Zimbabwe Harare. Mapema leo magari ya kijeshi na wanajeshi, wakionekana kuelekeza au kuzuia magari.

Emmerson Mnangagwa ni nani?

Akaunti ya chama cha Zanu PF inasemama kuwa Emmerson Mnangagwa amefanywa kuwa rais wa mpito. Mnangawa mwenye umri wa miaka 75 alifukuzwa kazi ya Makamu wa rais kutokana na kile serikali ilisema kuwa kutokuwa mtiifu.

Kufutwa kwake kulionekana kama nia ya kumwezesha mke wa Rais Mugabe, Grace, kufuata nyayo za mumewe na kuwa kiongozi wa Zimbabwe.

Awali alikuwa ametoa wito kwa mumewe kumfuta makamu wa rais. Mnangagwa ambaye ni mku wa zamani wa ujasusi amekuwa mtu ambaye alitarajiwa kumrithi Rais Mugabe 93.

Kufutwa kwake kulimaanisha kuwa Grace Mugabe anatarajiwa kuteuliwa kuwa makamu wa rais wakati wa mkutano maalum wa chama tawala cha Zanu-PF mwezi ujao.

Mugabe anajiandaa kuondoka madarakani

Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe anajiandaa kuondoka madarakani saa chache baada ya jeshi la Zimbabwe kutwaa madaraka, kwa mujibu wa mtandao maarufu wa habari nchini Afrika Kusini.

“Mugabe anajiandaa kuondoka madarakani,” mtandao wa wa News24 uliandika bila ya kutoa taarifa zaidi.

Misukusuko ya kisiasa imekuwa ikiongezeka tangu Mugabe hivi majuzi amfute Emmerson Mnangagwa, mshirika wake wa miaka mingi kama makamu wa Rais.

Mzozo wa Zimbabwe

Jeshi la Zimbabwe lilisoma taarifa kwenye kituo cha runinga cha serikali ZBC, likisema kuwa linachukua hatua ya kuwalenga wahalifu.

Hata hivyo limesema kuwa hayo sio mapinduzi ya kijeshi na Rais Mugabe yuko salama. Milio mikubwa ya risasi ilisikika katika maeneo ya kaskazini mwa mji mkuu Harare mapema leo.

Taarifa hiyo ya jeshi ilikuja saa kadhaa baada ya jeshi kudhibiti kituo cha ZBC.

Mwanamume mmoja ambaye alikuwa amevaa sare za jeshi alisema kuwa jeshi linataka kukabiliana na watu ambao wanatenda uhalifu unaoleta madhara ya kijamii na kiuchumi nchini Zimbabwe.

“Wakati tutakapomalzia wajibu wetu, tunatarajia kuwa hali itadudi kuwa sawa.” Taarifa hiyo ilisema kuwa Mugabe 93, na familia yake wako salama.

Haijulikani ni nani anaongoza hatua hiyo ya kijeshi. Magari ya wanajeshi waliojihami kwa silaha yanaonekana maeneo ya mjini Harare.

Hali hiyo ya wasi wasi wa lolote kuweza kutokea, imeanza hapo jana jioni, ambapo wanajeshi wakiwa na silaha walionekana wakijipanga katika maeneo kadhaa pamoja na kuzingira ofisi za shirika la utangazaji la Zimbabwe ZBC.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Kimataifa

Mahakama yamkuta na hatia Donald Trump

Spread the love  ALIYEKUWA Rais wa Marekani, Donald Trump, amekutwa na hatia...

Kimataifa

Harusi yageuka msiba 100 wakifariki kwa ajali ya moto

Spread the love  WATU takribani 100, akiwemo bibi na bwana harusi, wamefariki...

Kimataifa

Kampuni ya mali ya China Oceanwide yapata agizo la kufilisiwa huko Bermuda

Spread the love  MAHAKAMA ya Bermuda imetoa amri ya kufilisiwa kwa Kamapuni...

Kimataifa

Uvamizi wa kijeshi Milango ya bahari ya Taiwan G7 yapinga China

Spread the loveMKUTANO wa Mawaziri wa Mambo ya nje wa nchi za...

error: Content is protected !!