
Wapiganaji nchini DRC
WACHUNGUZI wa Umoja wa Mataifa wanaochunguza mauaji ya wataalam wao nchini DRC wamebaini kwamba wanajeshi wa serikali ya hiyo wanahusika na mauaji hayo, anaandika Catherine Kayombo.
Awali, ripoti ya wachunguzi hao kwa baraza la usalama la umoja wa mataifa halikueleza moja kwa moja kwamba wanajeshi hao wanahusika, bali imewaambia upelelezi unaendelea.
Wataalam hao wa umoja wa mataifa, Michael Sharp mwenye uraia wa Uswis na Zaida Catalan mwenye raia wa Chile waliuwawa mwezi Machi mwaka huu walipokuwa wakifanya utafiti kuhusu hali ya usalama nchini Congo.
Wakati huo huo, maofisa usalama nchini humo wanasema bado hawajafanikiwa kuwapata Mapadri wawili wa Kanisa Katoliki waliotekwa na watu wasiofahamika.
Hali ya usalama nchini Congo DRC imeendelea kupungua huku serikali ya Kinshasa ikiwashutumu waasi wa Kamwina Nsapu kwa mauaji ya wataalamu hao.
More Stories
Kenyatta awahakikishia viongozi wa dini amani makabidhiano ya madaraka
Seneta Mmarekani ayewapatanisha Uhuru, Raila atua Kenya
Ruto: Machifu, watumishi ‘waliotekwa’ upinzani warejee kazini