December 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

UN waumizwa na uamuzi wa TZ

Balozi Augustine Mahiga, Waziri wa Katiba na Sheria

Spread the love

TUME ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa (UN), imeitoa wito kwa Serikali ya Tanzania kutathimini upya, uamuzi wake wa kuzuia asasi za kiraia na raia, kufungua kesi kwenye Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu (AfCHPR). Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Tume hiyo imetoa wito huo jana tarehe 3 Desemba 2019 kupitia ukurasa wake wa twitter.

Taarifa ya tume hiyo imeeleza kuwa, mahakama ni muhimu katika mchakato wa haki na uwajibikaji nchini Tanzania.

“Tumeumizwa na uamuzi wa serikali ya Tanzania kuzuia mashirika yasiyo ya kiserikali (NGO’s), kupeleka kesi katika Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu.

Tunahimiza serikali kufikiria tena. Mahakama ni muhimu kwa haki na uwajibakaji nchini Tanzania,” inaeleza taarifa ya tume hiyo.

Madai ya Tanzania kutaka kujitoa katika mahakama hiyo yaliibuka hivi karibuni, na kupeleka Balozi Augustine Mahiga, Waziri wa Katiba na Sheria kutoa ufafanuzi wa suala hilo.

Katika ufafanuzi wake, Balozi Mahiga alisema Tanzania haijajitoa, bali imeomba kubadilisha itifaki kwenye mahakama hiyo, kwa madai kwamba inakinzana na sheria za Tanzania.

Balozi Mahiga alisisitiza kwamba, kama itifaki hiyo ambayo hakuihataja, haitarekebishwa, Tanzania itajitoa kwenye mahakama hiyo.

error: Content is protected !!