August 18, 2022

Uhuru hauna Mipaka

UN kumng’oa rais king’ang’anizi Gambia

Yahya Jammeh, Rais wa Gambia aliyeangushwa katika uchaguzi Mkuu

Spread the love

BAADA ya ujumbe wa marais wa Afrika Magharibi kushindwa kumshawishi Yahya Jammeh, Rais wa Gambia aliyeangushwa katika uchaguzi mkuu wa Disemba Mosi mwaka huu, Umoja wa Mataifa (UN) umesema hautamvulia abaki madarakani kibabe, anaandika Wolfram Mwalongo.

Ujumbe maalum uliowasili nchini Gambia tarehe 12 Disemba mwaka huu ukiongozwa na Ellen Johnson Sirleaf Rais wa Liberia pamoja na viongozi kutoka Nigeria na Ghana umeshindwa umemaliza mazungumzo na Jammeh huku rais huyo akigoma kuondoka madarakani.

“Tulikuja kuwasaidia watu wa Gambia lakini imeshindikana ingawa si jambo tunaloweza kulifanya kwa siku moja tu. Tutaendelea kulishughulikia jambo hili,” alisema Bi. Ellen.

Aidha Muhammadu Buhari, Rais wa Nigeria amewambia wanahabari mjini Banjul kuwa, Jammeh aliwapokea vizuri na kuwasikiliza lakini muafaka haukupatikana katika majadiliano hayo.

Mohamed Chambas mwakilishi wa Umoja wa Mataifa, Afrika Magharibi, amesema Jammeh anapaswa kukabidhi madaraka ifikapo Januari mwakani huku akisisitiza kuwa UN haitavumilia marais wanaoshindwa katika chaguzi na kubaki madarakani kwa nguvu.

“Ni matumaini yetu kwamba katika kipindi hiki majukumu yake yatatazingatia masharti na matakwa ya Katiba,” amesema.

Wiki iliyopita, Rais Jammeh alitangaza kutoyatambua matokeo yaliyo tangazwa na tume ya uchaguzi ya Gambia, baada ya tume hiyo kumtangaza Adama Barrow mshindi kwa kura 263,515 dhidi ya Jammeh aliyepata kura 202,099.

Ban ki Moon Katibu Mkuu wa UN anayemaliza muda wake amelaani kitendo cha rais huyo kuwafukuza kazi watendaji wa umma ambao hawakubaliana na uamuzi wa Jammeh kupinga matokeo halali ya uchaguzi.

error: Content is protected !!