UMOJA wa Wazazi wa CCM Tanzania, wamedai watahakikisha Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM, John Magufuli anakuwa rais wa serikali ya awamu ya tano ya Tanzania. Anaandika Hamisi Mguta … (endelea).
Katibu Mkuu wa Umoja wa Wazazi Tanzania, Seif Shabaan amesema watashiriki kusimamia mchakato wa uchaguzi mkuu ili kuhakikisha ushindi na unapatikana kwa amani wakati wa uchaguzi.
Shabaan amesema juhudi za kusimamia harakati zote za uchaguzi Mkuu na kuhakikisha ushindi wa CCM zilianza Februali 22-24 mwaka huu katika kikao kilichofanyika Dodoma, kilichoandaa mikakati tofauti ya ushindi.
Pia amesema wameanza kupeleka viongozi na watendaji kwenye kanda mbalimbali kusimamia shughuli zote za kampeni ikiwemo kanda za Pwani, Kati, Kaskazini, Kusini, Pemba na Unguja.
Hata hivyo amesema juhudi hizo zitafuta upotevu wa kura za chama tawala na kuwaelimisha watanzania waelewe umuhimu wa kupiga kura, kutokana na kile kilichoelezwa kuwa wapo wanaouza kura zao kwa bei poa na kupoteza haki ya kupiga kura.
Sambamba na hayo, Shabaan ametoa wito kwa watakaopiga kura kurejea majumbani mwao mapema baada ya kumaliza kupiga kura katika vituo husika, kwani kura zao hazitaibiwa kutokana na usimamizi ulioandaliwa.
More Stories
Chadema wamng’ang’ania Spika Tulia ajiuzulu
Viongozi CHASO wataja sababu za kuikacha kuhamia ACT-Wazalendo
LHRC yataja mwarobaini changamoto mchakato wa katiba kuvurugwa na wanasiasa