July 29, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Ummy Mwalimu: sheria ya ndoa ya 1971 irekebishwe

Spread the love

BAADA  ya Mahakama Kuu nchini kubatilisha ndoa ya chini ya umri wa miaka 18 ya mtoto wa kike wiki iliyopita , Ummy Mwalimu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto amethibitisha nia ya kupeleka muswada wa sheria mpya ya ndoa, anaandika Hamisi Mguta.

Mwalimu, amesema anatarajia kuwashilisha muswada wa marekebisho ya sheria ya Ndoa ya Mwaka 1971 bungeni ili kuweza kufikia azma ya kuwalinda watoto dhidi ya ndoa za utotoni.

Mwalimu ameyasema hayo leo wakati akizindua maadhimisho ya siku ya watu Duniani ambayo kitaifa yamefanyika jijini Dar es Salaam chini ya shirika la Umoja wa Mataifa Linaloshughulikia Idadi ya Watu Dunia – Tanzania(UNFPA) na mashirika mbalimbali yasiyo ya kiserikali.

“Marekebisho hayo nia pamoja na kifungu cha 13 na 17 vinavyotoa mwanya wa mtoto wa kike kuolewa katika umri mdogo wa chini ya miaka 18.

“Pamoja na sheria nzuri zitakazokuwepo, tatizo la mimba za utotoni  halitakwisha kama jamii haitabadilika kuhusu mtizamo hasi walio nao baadhi ya watu kuhusu wasichana,” amesema Mwalimu.

Amesema, Tanzania ni nchi inayoongoza kwa idadi kubwa ya matukio ya ndoa na mimba za utotoni ambapo matendo hayo kutendwa katoka mikoa ya Tabora, Katavi, na Simiyu, ikiwa  Dar es Salaam pamoja na Kilimanjaro zikifanya vizuri katika utoaji wa elimu kwa jamii.
Mwalimu ameahidi kusimamia haki za watoto wa kike  utoaji wa elimu.

“Suala kubwa ambalo nitahakikisha nalisimamia ni pamoja na kuhakikisha elimu ya afya ya uzazi mashuleni kwa watoto wetu, zama zimebadilika hakuna kusema tunawafundisha mambo makubwa mapema.

“Wanatakiwa kujua madhala ya ndoa za utotoni na masuala ya husuyo uzazi na tayari nimeshaomba kukutana na waziri wa elimu kupitia mtaala na kujua jinsi gani tutaongeza nguvu katika hili,”amesema.

error: Content is protected !!