Sunday , 29 January 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Ummy Mwalimu: Kuna vidudu mtu wa elimu bila malipo, Ma-RC, DC nimewaminya kidogo!
Habari za SiasaTangulizi

Ummy Mwalimu: Kuna vidudu mtu wa elimu bila malipo, Ma-RC, DC nimewaminya kidogo!

Ummy Mwalimu, Waziri wa TAMISEMI
Spread the love

 

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Ummy Mwalimu amesema kuna vidudu mtu ambao wanaeneza kwamba mpango wa elimu bila malipo kwa shule za msingi na sekondari unakwenda kufa jambo ambalo si kweli. Anaripoti Mwandishi Wetu, Kilimanjaro … (endelea).

Ummy Mwalimu ametoa kauli hiyo leo tarehe 15 Oktoba, mwaka huu wakati akizungumza katika mkutano wa ziara ya Rais Samia Suluhu Hassan ambaye yupo Mkoani Kilimanjaro kwa ziara ya siku mbili.

Amesema kwa miezi sita aliyokaa madarakani Rais Samia, mkoa wa Kilimanjaro tayari umepokea Sh bilioni 9.7 kutekeleza mango huo kwenye shule za msingi na sekondari.

“Elimu bila malipo chini ya Rais Samia itaendelea. Madiwani Moshi wameshapokea kiasi cha Sh bilioni mbili kwa ajili ya elimu bila malipo, milioni 62 elimu ya msingi, sekondari ni bilioni 1.9. Tupuuze maneno ya watu wasioipendea mema Tanzania,” amesema.

Aidha, amesema kila jimbo la mkoa wa Kilimanjaro kwa upande wa elimu, linakwenda kupata shule moja ya thamani ya Sh milioni 600 ambayo itakuwa imekamilika kila kitu.

“Waziri wa fedha amenieleza hizi fedha ndani ya wiki mbili tatu, zitakuja.

Aiidha, amesema kupitia fedha za mpango wa maendeleo na ustawi wa mapambano dhidi ya Corona, mkoa wa Kilimanjaro utapatiwa Sh bilioni nane kati ya hizo Sh bilioni 1.8 zinaelekezwa kwenye Halmashauri Moshi vijijini kujenga madarasa 85.

“Niwaombe wana Kilimanjaro hata mimi natamani sana 2025 ifike kama kesho kwa sababu Rais Samia anabebwa na kazi zake na mambo makubwa anayoyafanya chini ya kipindi chake kifupi cha uongozi,” amesema.

“Nimewaambia wakuu wa mikoa, wilaya na wakurugenzi, hivi wewe unapotaka kwenda kuzurura mikoa mingine wakati una madarasa 80 ya mpigo hujui yanaenda kujengwa wapi, ujenzi unaanza lini… kwa hiyo nimewaminya kidogo, nafahamu kuna wengine watakuja kwako, lakini kubwa nataka nisikuangushe, watoto wote waingie darasani Januari,” amesema.

Aidha, amesema barabara zenye urefu wa Kilomita 402 zitajengwa kwa kiwango cha changarawe tofauti na mwaka jana ambazo zilikuwa Kilomita 102.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Haya hapa matokeo ya mtihani kidato cha nne 2022

Spread the loveBARAZA la Mitihani la Tanzania (Necta) leo Jumapili limetangaza matokeo...

Habari za Siasa

NCCR-mageuzi yawaangukia Polisi kupotea kwa kada wake

Spread the loveJESHI la Polisi nchini limeombwa kufanya uchunguzi wa kina utakaosaidia...

HabariTangulizi

Bakwata wamkangaa Sheikh wa Dar es Salaam

Spread the love  BARAZA la Ulamaa, limefutilia mbali uamuzi wa “kuvunja ndoa,”...

Habari za Siasa

Uamuzi kesi ya kupinga Bodi ya Wadhamini NCCR-Mageuzi kutolewa Februari 6

Spread the love  MAHAKAMA Kuu, Masjala Kuu ya Dar es Salaam, imepanga...

error: Content is protected !!