June 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Ummy aonya watendaji afya

Spread the love

WATENDAJI wa serikali katika sekta ya afya wametakiwa kuwajibika ipasavyo kwa kutoa taarifa sahihi kuhusu idadi ya wagonjwa wa kipindupindu nchini. Anaandika Eunice Laurian.

Ummy Mwalimu ambaye ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto amesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati akitoa kuhusu mwenendo wa ugonjwa wa kipindupindu na tahadhari ya ugonjwa wa Zika nchini.

“Mojawapo wa changamoto katika mapambano ya kudhibiti mlipuko huu wa kipindupindu ni utoaji wa idadi pungufu au kutotoa kabisa taarifa za wagonjwa wa kipindupindu hivyo kupelekea kutokuwa na mafanikio katika mikakati iliyowekwa,” amesema Mwalimu.

Aidha, ametoa wito kwa sekta nyingine kushirikiana na wizara kupambana na ugonjwa huo ili kukabiliana na baadhi ya changamoto zinazowakabili watoa huduma za afya na elimu walioko katika maeneo mbalimbali nchini.

“Jukumu la kupambana na mlipuko wa ugonjwa huu si la Wizara ya Afya pekee naomba sekta nyingine ikiwemo Maji, Miondombinu, Biashara Elimu na Mazingira tushirikiane kwa pamoja ili kuutokomeza ugonjwa huu.” amesema.

Mwalimu   ameeleza kuwa, takwimu za kuanzia tarehe 1 hadi 7 Februari mwaka huu zinaonesha kuwa, idadi ya wagonjwa wa kipindupindu imepungua kutoka 459 ya wiki iliyoisha tarehe 31 Januari hadi 258 ambapo ni sawa na punguzo la asilimia 44.

Hata hivyo amesema wizara imewatoa hofu wananchi na kuwakumbusha kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa Homa ya Zika pamoja na magonjwa mengine yanayoenezwa na mbu.

error: Content is protected !!