Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Umeya, Uenyekiti: La mgambo limelia CCM
Habari za Siasa

Umeya, Uenyekiti: La mgambo limelia CCM

Humphrey Polepole, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM
Spread the love

HALMASHAURI Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (NEC-CCM), imefanya uteuzi wa wagombea nafasi za Meya wa Jiji, wenyeviti wa Halmashauri za Wilaya na Miji. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Taarifa hiyo imetolewa leo Ijumaa tarehe 20 Novemba 2020 na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole wakati akitoa taarifa ya kikao cha NEC, kilichofanyika jana tarehe 19 Novemba mwaka huu.

Polepole amesema, majina ya wagombea hao yatakwenda katika mchujo wa mwisho katika Kamati za Madiwani wa CCM.

“NEC iliketi kufanya uthibitisho wa uteuzi wa wagombea nafasi za Meya wa Jiji sita, wenyeviti wa halmashauri za wilaya na miji,”amesema Polepole.

Amesema, NEC imeagiza Kamati za Mdiwani wa chama hicho kufanya uchaguzi wa wagombea nafasi za umeya wa halmashauri za jiji na manispaa pamoja na wenyeviti wa halmashauri za wilaya na miji, watakaokwenda kushindana na wagombea wa vyama vya upinzani.

Amesema, uchaguzi huo ufanyike tarehe 23 hadi 24 Novemba 2020.

“Hawa wote nilio watamka kamati za madiwani wa CCM watafanya uchaguzi kumpata mgombea wa CCM atakayeshindana na wagombea wa upinzani wa halmashauri za baraza la madiwani  kuanzia Jumatatu, kamati za madiwani ziketi kote nchini kwa niaba ya kamati kuu. Uchaguzi huo ufanyike na tunaanza Jumatatu na Jumanne,” amesema Polepole.

Polepole amesema NEC imeagiza wajumbe wa kamati za madiwani wa CCM katika maeneo husika kuchagua watu watakaowezalinda masilahi ya umma.

“Kuhakikisha uchaguzi unakwenda vizuri na kamati kuu imeiridhisha yoyote atakayepatikana, atalinda maslahi ya umma,” amesema Polepole.

Akielezea uteuzi huo, Polepole amesema kuna sehemu NEC ilifanya uteuzi wa jina moja la mgombea huku maeneo mengine ikiteua jina zaidi ya moja.

“Halamshauri Kuu imerudisha jina moja ambalo wanaona anaweza kulinda maslahi ya umma, yako maeneo kamati kuu imerudisha watu wawili na yako maeneo tumerudisha watatu, tumesema hao waende wakatekeleze demokrasia pana zaidi,” amesema Polepole.

Polepole amesema, katika Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam wagombea waliojitokeza kuomba kuteuliwa na NEC kugombea U-Meya ni tisa, Arusha (17), Dodoma (7), Tanga (6), Mwanza (7) na Mbeya (10).

Kwa upande wa Halmashauri za Manispaa, Polepole amesema nafasi zilizo gombaniwa ni 20 na waliojitokeza kusaka nafasi hizo walikuwa  150.

Wakati wanachama wa CCM  682 kusaka nafasi 137 za uenyekiti wa halmashauri za wilaya, huku watu 109 walijitokeza kusaka nafasi 22 za uenyekiti wa halmashauri za miji .

Hata hivyo, Polepole amesema kuna baadhi ya halmashauri mchakato wa uteuzi wa meya na wenyeviti wa halmashauri haukufanyika, ikiwemo Halmashauri ya Wilaya ya Njombe na Nyasa. Halmashauri ya Mji wa Nzega

Amesema, NEC ameagiza maeneo ambayo uteuzi haukufanyika kurudia mchakato huo upesi.

CCM ilifungua pazia la uchukuaji na urudishaji fomu za kugombea U-Spika, Meya na Uenyekiti wa Halmashauri kuanzia tarehe 2 hadi 3 Novemba mwaka huu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MWANACHAMA wa Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, amedai...

Habari za Siasa

Wabunge waikalia kooni TAKUKURU Bungeni

Spread the love  BAADHI ya wabunge wamelia na changamoto za utendaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Mpina ataka Waziri Majaliwa ajiuzulu, akosoa teuzi za mawaziri

Spread the love  MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina, amemtaka Waziri Mkuu, Kassim...

error: Content is protected !!