July 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Umeme `wasitisha` safari za ndege Mwanza

Uwanja wa Ndege wa Mwanza

Spread the love

ABIRIA wanaotumia usafiri wa anga mkoani Mwanza, wameilalamikia Mamlaka ya viwanja vya ndege Tanzania (TAA) nchini , kushindwa kutafuta njia mbadara ya kutatua kero ya umeme inayoendelea hivi sasa. Anaandika Moses Mseti, Mwanza … (endelea).

Tatizo la umeme katika uwanja wa ndege wa Mwanza limekuwa kero kubwa kwa abiria wanaowasili na kuondoka hususani nyakati za usiku ambako umeme unapokuwa umekatwa na Tanesco.

Akizungumza na Mwanahalisi online Mmoja wa abiria, Diana Anthony,amesema amelazimika kusitisha safari kutoka Mwanza –Dar es salaam kutokana na tatizo la uwanja huo kukosa huduma ya umeme.

Amesema kitendo cha mamlaka ya ndege nchini kushindwa kutafuta njia mbadala pindi umeme unapokuwa umekatwa nidhahiri mamlaka hiyo imeonesha uzembe wa hali ya juu.

“Hivi hii Nchi yetu tanakoelekea ni wapi jamani, kweli uwanja mkubwa kama huu unashindwa kuwa na jenereta? ndege inaposhindwa kutua na kuondoka uwanjani hivi hawafahamu kama taifa linakosa mapato.

“Maeneo ambayo ni mhimu kama Hospitalini na viwanja vya ndege hayapaswi kukosa umeme na kama utakosekana wanapaswa kuwa na jenereta za ambazo ni za uhakika,” amesema Anthony

Anthony amesema kukosekana kwa umeme katika maeneo hayo nyeti kunaweza kusababisha watu wenye nia mbaya kufanya vitendo vya kiuhalifu.

Meneja wa Uwanja wa Ndege wa Mwanza, Ester Madale, amesema tatizo la ndege kutotua nyakati za usiku uwanjani hapo linatokana na umeme jijini humo.

Madale amesema tatizo hilo halipingiki kutokana na kuwepo na katizo la umeme hapa nchini hivyo ni bora abiria wakawa wavumilivu katika kipindi hiki.

“Hivi karibuni ndege ya Fastjet haikuweza kutua kwa sababu ya tatizo la umeme, kuhusiana na jenereta anahusika mkuu wangu wa kazi ambaye anaweza kukuelekeza,” amesema Madale.

Hata hivyo inaelezwa licha ya uwanja huo wa ndege kuwa na jenereta inadaiwa wameshindwa kununua mafuta na kutumia jenereta hizo ili kuweza kukabailiana na hatari yoyote ambayo inaweza kutokea.

error: Content is protected !!