October 2, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Umeme kukatika Dar es Salaam

Mafundi umeme wakiwa kazini

Spread the love

SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO), limetangaza katizo la umeme katika baadhi ya maeneo ya Wilaya ya Ilala na Temeke, jijini Dar es Salaam. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Kwa mujibu wa tangazo hilo, katizo hilo litatokea kesho tarehe 22 Oktoba 2019, kuanzia saa 2:30 asubuhi hadi 10:30 jioni, kwenye njia ya Msongo wa 132KV ili kuruhusu kazi ya kuungwa kebo ya Transfoma mpya.

Tangazo hilo limeeleza kuwa, Transfoma hiyo mpya ina uwezo mkubwa wa Megawati 300MVA, ambayo itasaidia kuboresha hali ya upatikanaji wa umeme kwa Jiji la Dar es Salaam, Zanzibar na Pwani.

Maeneo yatakayokumbwa na katizo hilo ni pamoja na, Buguruni, Vingunguti, Tazara, Gongo la Mboto, Ukonga, Mombasa, Mzambarauni, Pugu.

Maeneo mengine ni Yombo, Kitunda, Machimbo, Mwanagati, Mbondole pamoja na baadhi ya maeneo ya Tabata.

error: Content is protected !!