Friday , 29 March 2024
Home Habari Mchanganyiko UMACHEDO waja na tahadhari ya corona
Habari Mchanganyiko

UMACHEDO waja na tahadhari ya corona

Mwenyekiti wa Umoja wa Mafundi Cheleani wa Dodoma (UMACHEDO), Khalid Zoya
Spread the love

UMOJA wa Mafundi Cherehani Mkoa wa Dodoma (UMACHEDO), umewataka mafundi wote kuchukua tahadhari katika kujikinga na virusi vya corona (COVID-19), ambavyo kwa sasa ni tishio duniani. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Akizungumza na vyombo vya habari leo tarehe 27 Machi 2020, Khalid Zoya ambaye ni mwenyekiti wa umoja huo mafundi wa kushona wanakutana na watu wengi hivyo amewataka kuwa na tahadhari.

Zoya amesema, ni vyema kila fundi mahali alipo akahakikisha anakuwa na vifaa vya kujikinga na maambukizi ya virusi hivyo, ikiwa ni pamoja na kuwa na vitakatisha mikono.

Amesema, ametoa maagizo kwa mafundi wote wa cherehani kuhakikisha, wanatoa elimu kwa wateja wao juu ya kujikinga na maabukizi hayo.

“Sisi mafundi cherehani tunakutana na watu wengi na wa aina mbalimbali, kutokana na hali hiyo, tunatakiwa kuwa na tahadhari kubwa ya kujikinga na maambukizi.

“Lakini si hilo tu, nimewaagiza mafundi wote ambao ni wanachama kuhakikisha wanakuwa na vitakatisha mikono katika maeneo yao ya kazi, ili kuweza kutekeleza agizo la serikali la kujikinga na virusi hivyo,” amesema na kuongeza:

“Ikumbukwe kuwa ugonjwa huu siyo wa kufanyia mzaa hata kidogo tumeshuhudia mataifa makubwa na yenye uchumi mkubwa yakiangaika  hivyo basi ni lazima na sisi watanzania tukawa makini na jambo hili bila kulifanyia alisema.”

Pia mwenyekiti huyo amesema, ametoa maagizo wa viongozi wa chama hicho waliopo wilayani kuhakikisha wanatoa elimu kwa jamii inayowazunguka pamoja pamoja na mafundi wenyewe.

“Huko wilayani hususani vijijini, nimewaelekeza viongozi wangu kuhakikisha wanawatembelea mafundi cherehani  kutoa elimu juu ya kujikinga na gonjwa hili hatari,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mtandao watetezi wa haki za mazingira Tanzania waundwa

Spread the loveMTANDAO wa watetezi wa haki za mazingira nchini Tanzania, umeundwa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga kuongoza usambazaji wa mitungi ya gesi 10,000 ya Taifa Gas

Spread the loveNaibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga ameahidi kuongoza kwa ufanisi...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyabiashara, wawekezaji China waridhia kuwekeza bil. 800 katika sekta 5 nchini

Spread the loveUJUMBE wa wafanyabiashara na wawekezaji wakubwa kutoka Jimbo la Changzhou...

Habari Mchanganyiko

Bil. 4.42 kumaliza uhaba maji kata 2 Musoma Vijijini

Spread the loveWANANCHI wa kata za Busambara na Kiriba, Jimbo la Musoma...

error: Content is protected !!