Wednesday , 29 March 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Umaarufu wa Rais Magufuli waiponza Twaweza
Habari za SiasaTangulizi

Umaarufu wa Rais Magufuli waiponza Twaweza

Spread the love

SERIKALI ya Tanzania imeitaka taasisi ya utafiti isiyo ya kiserikali ya Twaweza kueleza ni kwa nini ilifanya utafiti kuhusu maoni ya wananchi ‘bila kibali’. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea). 

Tume ya Sayansi na Teknolojia (Comstech) imeiandikia taasisi barua na kuitaka ieleze ni kwa nini haifai kuchukuliwa hatua za kisheria.

Barua hiyo inasema Twaweza waliwasilisha maombi ya vibali vya kufanya utafiti awali nchini Tanzania lakini utafiti huo wa Sauti ya Wananchi haukujumuishwa.

“Mwishoni mwa wiki kulikuwa na taarifa kuhusu utafiti mpya wa Twaweza kwa jina Sauti za Wananchi.

“Kwa kuwa tume hii haina rekodi zozote kwamba ilitoa kibali kwa Twaweza au kuna ombi la kibali cha utafiti kama huo ambacho kiliwasilishwa, kuchapishwa kwa matokeo ya utafiti huo kunakiuka kifungu 11 cha Mwongozo wa Kusajiliwa na Kuidhinishwa kwa Usajili wa Kitaifa kwa kutoandikisha mradi huu wa utafiti kwa Soctech.”

Twaweza wamethibitisha kwamba wameipokea barua hiyo lakini bado hawajatoa tamko rasmi.

Utafiti huo wa Twaweza ulikuwa unasema asilimia 65 ya wananchi Watanzania walisema hawako tayari kutumia njia ya maandamano kuishinikiza serikali katika mambo yasiyowaridhisha.

Kwa upande mwingine, mwananchi mmoja kati ya wanne (27%) ana uwezekano wa kushiriki kwenye maandamano.

Ikilinganishwa na takwimu za mwaka 2016, idadi ya wanaosema wana uwezekano wa kushiriki ilishuka kidogo sana (kutoka 29% mpaka 27%) wakati ambao wanasema hawana uwezekano wa kushiriki imeongezeka (kutoka 50% mpaka 65%).

Wananchi wachache kwa hiari walitaja maandamano kama njia ya kufikisha malalamiko yao kwa serikali. Idadi kubwa ya wananchi walisema hawako tayari kushiriki kwenye maandamano kuhusu jambo lolote lisilowapendeza.- ikiwemo idadi kubwa ya wafuasi wa vyama vya upinzani.

Na wananchi wengi zaidi wanaunga mkono serikali kukataza mikutano na maandamano ya kisiasa kuliko wale wanaopinga.

Utafiti wa Twaweza ulitaja sababu kadhaa za kutofanyika maandamano ya tarehe 26 mwezi Aprili mwaka 2018 kama yalivyokuwa yamepangwa na mwanaharakati Mange Kimambi.

Utafiti huo pia ulibaini kuwa umaarufu wa Rais John Magufuli umeshuka kutoka asilimia 96 mwaka 2016 hadi kufikia asilimia 55 mwaka huu.

Asilimia 55 ya wananchi wanaukubali utendaji wa Rais Magufuli tangu alipoingia madarakani mwaka 2015. Kukubalika huku kumepungua kutoka 96% mwaka 2016, na 71% mwaka 2017.

Kiwango cha kukubalika kwa Rais kimeshuka kutoka kwenye rekodi ya juu kuwahi kuwekwa na Rais wa Tanzania mpaka rekodi ya chini tangu takwimu hizi zianze kukusanywa mwaka 2001.

Msemaji na katibu mwenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Humphery PolePole alikosoa utafiti huo wa Rais Magufuli bado ni maarufu sana nchini Tanzania kutoka na sera zake.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

DC Kasilda Mgeni ahamasisha chakula shuleni

Spread the love  MKUU wa Wilaya ya Same, mkoani Kilimanjaro, Kasilda Mgeni...

Habari za Siasa

Bilioni 223.9 zapelekwa Tunduru ndani ya miaka 2 ya SSH

Spread the love  ZAIDI ya Sh. bilioni 223.9 zimepelekwa Wilaya ya Tunduru...

Habari za Siasa

Rais Samia aagiza iundwe kamati ya pamoja ya Mawaziri mradi wa BBT

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amewaagiza mawaziri kuunda kamati...

Habari za Siasa

Rais Samia apangua makatibu tawala mikoa, ateua Kamishna DCEA

Spread the loveALIYEKUWA Kamishna wa Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya, Gerald...

error: Content is protected !!