Tuesday , 23 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Ulinzi waimarishwa kesi ya kina Mbowe
Habari za Siasa

Ulinzi waimarishwa kesi ya kina Mbowe

Spread the love

 

JESHI la Polisi limeimarisha ulinzi ndani na nje ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam wakati kesi ya kiongozi wa chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania, Freeman Mbowe na wenzake watatu ilipokuwa ikiendelea. Anaripoti Victoria Mwakisimba, TUDACo … (endelea).

Mbowe na wenzake watatu, Halfan Bwire Hassan, Adam Hassan Kasekwa na Mohamed Abdallah Ling’wenya leo Jumatatu, tarehe 23 Agosti 2021, wamesomewa maelezo ya awali ya mashitaka yanayowakabili ya uhujumu uchumi na kupanga njama za kufanya ugaidi.

Pia, Mbowe anatuhumiwa kufadhili vitendo vya uhadi kwa kutoka zaidi ya shilingi laki sita.

Kabla na baada ya kesi hiyo mahakamani hapo, ulinzi umeimalishjwa na vikosi vya polisi wenye silaha mbalimbali pamoja na askari kanzu.

Askari wamejipanga ipasavyo ndani na nje ya viunga vya mahakama kuhakikisha hakuna uhalifu unaotokea wakati wa kesi hiyo ikiendelea huku wakihakikisha kila anayeingia anakuwa amefanyiwa ukaguzi ili kujua kama hajabeba kitu chochote hatarishi.

Lakini pia kuna askari polisi takribani mita 200 kabla ya kufika Mahakamani ambao pia lengo lao ni kuhakikisha zoezi linaendeshwa bila uvunjifu wowote wa amani, asilimia kubwa Askari hawana silaha zozote hali inayo ashiri kuwapo kwa amani eneo hilo.

Hata hivyo, wanachama na wafuasi wa Chadema waliofika mahakamani hawakuwa wengi.

Endelea kufuatilia MwanaHALISI TV, MwanaHALISI online na mitandao yetu ya kijamii kwa habari na taarifa mbalimbali

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

Habari za Siasa

Serikali kuanzisha mradi wa Gridi ya maji ya Taifa

Spread the loveWaziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema katika mwaka wa fedha...

Habari za SiasaTangulizi

Shibuda amlima waraka mzito Bulembo

Spread the loveMKONGWE wa siasa nchini, John Shibuda amemshukia kada maarufu wa...

error: Content is protected !!