
Dk. Harrison Mwakyembe, Waziri wa Wizara ya Katiba na Sheria
SHERIA ya kuwalinda watoa taarifa za uhalifu na mashahidi (The Whistleblower and Witness Protection Act. 2016) tayari imeanza kutumika, anaandika Pendo Omary.
Muswada wa Sheria hiyo ulipitishwa na Bunge la Tanzania, tarehe 25 Machi, Mwaka huu huku Dk. Harrison Mwakyembe, Waziri wa Wizara ya Katiba na Sheria akiidhinisha sheria hiyo kuanza kutumika kuanzia tarehe 1 Julai, mwaka huu.
Kamana Stanley, Mkurugenzi Msaidizi wa kitengo cha utekelezaji wa Katiba katika Wizara ya Katiba na Sheria, amewaambia waandishi wa habari leo kuwa, sheria hiyo itawabana watakaoshindwa kushughulikia taarifa zitakazotolewa na kuruhusu watoa taarifa kupata madhara.
“Sheria hii imeweka utaratibu wa kuwapatia motisha, wote wanaofanikisha kuokoa mali ya umma, kukamatwa kwa wahalifu, kulinda mazingira na maisha ya binadamu kutokana na taarifa walizotoa katika mamlaka husika,” ameeleza Stanley
Motisha kwa watoa taarifa hao itahusiha pia fidia kwa ambao wataathirika kutokana na taarifa walizotoa.
Kuwepo kwa Sheria hiyo kutasaidia kuwapatia ulinzi wa kisheria watoaji wa taarifa za uhalifu wa makosa ya aina mbalimbali.
Itarahisisha pia utoaji na upatikanaji wa taarifa si katika vyombo vya dola pekee bali hata kupitia vyombo vya habari na vyanzo vingine vinavyoainishwa katika sheria hiyo.
More Stories
Takukuru yavimbia wakandarasi, ‘yarejesha’ mil 420 Tanesco
IGP Sirro: Hatufungui kesi za madai, migogoro ya ardhi
Panyabuku waanza kubaini TB