July 1, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Ulimwengu awapa somo waandishi

Spread the love

MWANDISHI mkongwe nchini, Jenerali Ulimwengu amewataka wamiliki wa vyombo vya habari na waandishi kuipinga rushwa kwa vitendo hasa wakati huu wa uchaguzi mkuu. Anaandika Sarafina Lidwino … (endelea).

Amesema, waandishi wanapaswa kufuata maadili ya kazi yao badala ya kujirahisisha na kukubali kununuliwa na kwamba, matokeo yake wanaishia kuandika habari za upotoshaji.

Mkongwe huyo ametoa kauli hiyo le jijini Dar es Salaam wakati akiwasilisha mada kwenye kongamano la wadau wa habari Dar es Salaam (DCPC) lililofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Peacock na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali.

Kongamano hilo lililenga kujitathmini kwa waandishi juu ya utekelezaji wa maadili ya uandishi katika kipindi hiki cha uchaguzi pamoja na kujadili maoni mbalimbali kutoka kwa wadau wa habari.

Katika mada yake hiyo pia amesema, waandishi wa habari wanatakiwa kujua kuwa wao ndio daraja kati ya viongozi na wananchi na kwamba wanaweza kujenga au kupotosha.

“Tuache kununuliwa kwa bei rahisi maana wakishatununua lazima uwe chini yake na anakupeleka anavyotaka. Kazi yetu ni kama kazi za kiroho na sio ya mdhaha kwani tunawaongoza wananchi wengi ambao wanatuamini,” amesema.

Amesema, kuna baadhi ya vyombo vya habari vinapotosha umma kwa kubagua habari akitolea mfano Televisheni ya Taifa (TBC) licha ya me,bo yao kuelesa ‘Ukweli na Uhakikal’ na kuwa “ lakini bado inapotosha.”

Pia amesema, mwandishi anaweza kuwa upande wowote wa siasa ambao anautaka lakini aweke wazi na si kutumia habari za ukweli kupotosha umma kwa manufaa yake binafsi.

“Tuache kauli za chuki na matamko yanayochochea uvunjufu wa amani, tujenge tabia ya kusema ukweli penye ukweli na kama una mawazo yako binafsi ni vema uandike hata jina lako uweke na picha yako ili jamii ijue uko upande gani kuliko kutumia jina lingine ili kusababisha maumivu kwa wengine,” amesema Ulimwengu.

Meneja wa Maadili wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Allan Lawa kwenye kongamano hilo amesema, vyombo vya habari vinatakiwa kufanya mijadala na wagombea ili kuwapa fursa ya kueleza sera zao.

Amesema, waandishi wanatakiwa kuwa wabunifu wenye kuhoji na kudadisi ili kuweza kutoa elimu nzuri hasa elimu ya mpiga kura kwa jamii kuliko kuwapotosha.

“Ninauhakika baada ya uchaguzi kuna vyombo vya habari vitapoteza mwelekeo na ladha ya habari zao kani hivi sasa vinatumika vibaya,” amesema Lawa.

error: Content is protected !!