Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Ulimwengu: Anayezuia mjadala wa katiba mpya ni mfu kimawazo
Habari za SiasaTangulizi

Ulimwengu: Anayezuia mjadala wa katiba mpya ni mfu kimawazo

Jenerali Ulimwengu
Spread the love

 

MWANDISHI wa habari mkongwe nchini Tanzania, Jenerali Ulimwengu, amesema, mtu anayedhani marekebisho ya katiba yaliyofanyika 1977, yanakidhi matakwa ya uendeshaji wa nchi kwa sasa, amekufa kimawazo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Ulimwengu ametoa kauli hiyo leo Jumanne, tarehe 7 Desemba 2021, katika mdahalo wa kujadili kitabu chake cha Rai ya Jenerali Ulimwengu, uliofanyika ukumbi wa mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

“Ni mjinga peke yake anayedhani kazi iliyofanyika 1977 ya kufikiri namna ya kuendesha nchi hii inatosha, huyu mtu kimawazo ni mfu, ni maiti wa kimawazo, ingawaje anaonekana anatembea, lakini kimawazo huyu mtu ni maiti,” amesema Jenerali Ulimwengu.

Mchambuzi huyo wa masuala ya kisiasa nchini Tanzania, amesema suala la kujadili katiba mpya ni endelevu, kwani maisha ya binadamu yanabadilika kila wakati.

“Kwa hiyo, suala la kujadili katiba ni suala la kudumu, wala halihitaji kupangiwa vipindi kwamba kuanzia Desemba tutajadili katiba, mpaka ikifika Machi basi, hata kidogo.”

“Ni mjadala wa kudumu sababu tunataka kuborehsa namna tunavyeondesha shughuli zetu kama taifa na kila wakati kuna nafasi ya kuboresha,” amesema Jenerali Ulimwengu.

Mkuu huyo wa wilaya wa zamani wa Ilala jijini Dar es Salaam, amesema mjadala wa kudai katiba mpya lazima uwe wa uwazi mpana, kwani inahitaji marekebisho ya kila mara.

“Tuna uhuru wa kufikiri nje ya kile tunachoambiwa na watala na sisemi kuna watala wameshatuambia usifikiri kuhusu katiba mpya, tumeona tumejadili sana masuala ya katiba,” amesema Ulimwengu

“Lazima tuendelee kujadili haya masuala kwa uwazi mkubwa na tukijua hayaondoki, hayana majira au vipindi.”

“Hata tutakapoandika katiba mpya tukaipitisha wananchi wakaikubali, siku ya pili lazima tukae chini tuseme kati ya jana na leo kuna jambo limebadilika katika maisha yetu tunadhani katiba hii haitoshi kulishughulikia,” amesema

Ulimwengu amesema “tutaanza mjadala ili baada ya mwaka mmoja tuone kuna vipengele katika katiba iliyopitishwa mwaka jana inatakiwa kubadilishwa, ni jambo la kudumu kila wakati inatakiwa kuboreshwa.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Habari za SiasaTangulizi

Tanzania, Uturuki zanuia kukuza biashara, uwekezaji

Spread the loveSERIKALI za Tanzania na Uturuki zimekubaliana kuendeleza dhamira ya kuimarisha...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza ajira watendaji daftari wapiga kura

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza nafasi...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema yatangaza ruti awamu ya pili maandamano

Spread the love  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema awamu ya...

error: Content is protected !!